MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER UNITED imekamilisha usajili wake wa kwanza katika majira haya ya joto kwa kumpa mkataba wa miaka mitano beki wa Benfica, Victor Lindelof baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Beki huyo aliyeigharimu United Pauni 30.7 milioni, aliwasili kwenye viwanja vya mazoezi vya United, Carrington Jumatano asubuhi kabla ya kumwaga wino katika mkaba huo .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 22 alikuwa akiwandwa na Kocha wa Unityed Jose Mourinho tangu katika usajili wa Januari.
Lindelof amefurahia kutua Old Trafford ambako atakaa hadi mwaka 2021.
Pia, imefahamika kwamba klabu yake ya Benfica inaweza kupata bonasi ya Pauni 8.8 milioni kama beki huyo atafanya vizuri Old Trafford.
Akizungumza na mtandao wa klabu hiyo, Lindelof alisema: "Ninafuraha kubwa kujiunga na Manchester United. Nilifurahia kuwapo Benfica na nimejifunza mengi pale.
"Lakini ninaangalia mbele kucheza Ligi Kuu England uwanjani Old Trafford na kwa Jose Mourinho.
Lindelof akiwamwaga wino
"Nina kiu ya kuanza kutoa mchango wangu kwa timu ili kutwaa mataji zaidi,"alisema beki huyo anayefananishwa na beki za zamani wa timu hiyo, Rio Ferdnand na akitarajiwa kuwa pacha wa Eric Bailly.
Lindelof atapata nafasi ya kuitumikia timu yake hiyo mpya katika majira haya ya joto pindi United itakapofanya ziara maandalizi ya msimu, Marekani.
Akiwa katika viwanja vya mazoezi vya Man United.
Kocha Mourinho anaamini Lindelof ataongeza kitu katika safu yake ya ulinzi msimu ujao, ikizingatiwa kuwa timu hiyo itacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment