0
                                   MADRID, HIPSANIA
UNAKUMBUKA kile kilichomkuta Lionel Messi pale Hispania? Hata yale majanga yaliyomkuta beki, Javier Mascherano na Neymar baada kusajiliwa akitokea Santos ya kwao Brazil?
Basi wanasheria wa Hispania wamemshitaki straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa  kosa la kutowasilisha mamilioni ya Euro katika mamlaka ya kodi .
Ofisi ya waendesha mashtaka hiyo imesema imefungua kesi dhidi ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kwa ukwepaji huo wa kodi.
Ronaldo anatuhumiwa kuikosesha mamlaka ya kodi ya Hispania Euro14.7 milioni ( sawa na Pauni 13 milioni au Dola 16 milioni) kuanzia mwaka 2011 hadi 2014.
Katika ripoti iliyotolewa na wawakilishi wa nyota huyo wakulipwa ilisema hakukuwa na kificho wala lengo lolote na kukwepa kodi.
"Ni wazi kwamba Ronaldo hajajaribu kukwepa kodi," meneja wa mchezaji huyo wa  alisema .
Upande huo unasisitiza kwamba Ronaldo hajaficha taarifa zake za mapato kwa mamlaka ya kodi au kufanya udanganyifu juu ya jambo hilo tangu ameingia Hispania.


                      Ronaldo akiwa na Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya

Straika huyo ambaye hivi karibuni aliisaidia timu yake ya Real Madrid kushinda taji la Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya alisema hana wasiwasi na uchunguzi unaofanya kuhusu malipo ya kodi na hana cha kuficha.
Katika sakata hili, anashatakiwa kwa kujua kutumika kwa picha zake na kuficha mapato kutokana na haki zake zilizotokana na picha hizo.
Taarifa za jambo hili zilianza kuvuja tangu Desemba mwaka jana, lakini Ronaldo alikanusha kuhusika.
Alipohojiwa kuhusu uchunguzi huo, Ronaldo alimwambia mwandishi wa habari wa Runinga na Redio ya Ureno (RTP) kwa Lugha ya Kireno: "Quien no debe no teme", kwa tafsiri isiyo rasmi ilimaanisha: "Hana cha kuficha na haofii uchunguzi huo."
Ronaldo ni mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa mwaka wa pili mfululizo kwa mujibu wa Jarida la Forbes.

                                               Ronaldo akiitumikia Ureno
Staa huyo analipwa Dola 93 milioni ( Pauni 72 milioni) kutokana na mshahara, bonasi na uwekezaji wake wa aaina mbalimbali kwa mwaka jana.

Post a Comment

 
Top