SHANGHAI,
CHINA
CARLOS
Tevez anazeeka vizuri. Atakula pensheni kwa raha sana!
Unajua
kwa nini? Nikikwambia kile kilichovuja kwenye mkataba wake unaonyesha kiwango
cha pesa anacholipwa na klabu yake ya Shanghai Shenhua ya huko China, utapata
kizunguzungu.
Mambo
yamevuja bana na pesa anayolipwa Tevez haijawahi kulipwa kwa mchezaji yeyote
tangu sayari hii ya dunia ilipoanza, hata Cristiano Ronaldo na Lionel Messi
hawalipwi pesa kama hiyo, achana tu na wazo kwamba pengine watalipwa hata huko
baadaye.
Tevez
anapokea Pauni 634,615 kila wiki kama mshahara wake kwenye kikosi hicho cha
Shanghai Shenhua. Wakati ukiendelea kupiga hesabu zake kuichenji pesa hiyo kuwa
shilingi ya Kitanzania kujua anapokea kiasi gani kwa wiki, kwa taarifa yako tu,
Tevez anapokea Pauni 788,000 nyingine kama atacheza asilimia 70 ya mechi za
timu hiyo kwa msimu huu.
Ligi Kuu China ina timu 16, sawa na mechi 30
kwa msimu, hivyo Tevez akicheza mechi 21 tu, anavuna Pauni 788,000.
Ushapata
Pauni 788,000 sasa na shilingi ngapi za Kitanzania, kama ukienda kuchenji Pauni
1 sawasawa na Sh 2,800? Rahisi tu mwana, zidisha 788,000 mara 2800. Tena hapo
zile senti senti zimeondolewa, kwa sababu Pauni 1 ya Uingereza siyo Sh 2,800
kamili, ni Sh 2,853.
Tevez
atalipwa kiasi kama hicho tena, Pauni 788,000 kama timu yake itashinda taji la
ubingwa wa Ligi Kuu China na Pauni 1.56 milioni kama itanyakua ubingwa wa Ligi
ya Mabingwa Asia.
Messi
Si
unafahamu uwezo wa Tevez kwenye kupasia nyavu, basi kama ataendeleza makali
yake hayo China, atalipwa Pauni 390,000 kama atamaliza msimu akiwa kinara wa
mabao.
Bahati
mbaya kwa Carlos ni kwamba hana majaabu tangu alipotua kwenye soka hilo la
China. Kwa msimu huu kupata bonasi zinazotokana na kucheza asiliami 70 ya
mechi, kuwa kinara wa mabao, timu yake kuwa ubingwa wa ligi au bingwa wa Asia
ni ngumu kutokana na hali halisi. Kwa mwaka huu wa 2017, Tevez amefunga bao
moja tu katika mechi nne alizocheza, huku timu yake ikiwa kwenye nafasi ya tisa
katika msimamo wa ligi hiyo.
Ronaldo
Mahali
pekee kwenye uhakika wa mkwanja wake ni kwenye mshahara, kwa sababu ni lazima
alipwe mzigo wake hata kama atakuwa hajacheza mechi yoyote kwa wiki husika.
Hata hivyo, kwa upande wa mshahara, Tevez si mchezaji anayelipwa pesa nyingi
baada ya mambo kufichuka kuwa Ezequiel Lavezzi analipwa Pauni 800,000 kwa wiki
kutokana na huduma yake anayotoa Hebei China Fortune.
Lavezzi
Mzigo
mkubwa wa pesa zinazotolewa na klabu za Ligi Kuu China ndicho kinachoondoa
mshangao wa kumwona straika Diego Costa akiachana na maisha ya Chelsea mwishoni
mwa msimu huu na kutimkia huko Mashariki ya Mbali.
Lakini,
itakuwa vipi Tevez akidaka bonasi zote hizo, unadhani uzee wake utakuwaje?
Wachina si watu wa mchezomchezo!
Post a Comment