0


                  LONDON, ENGLAND
KWENYE mazoezi ya Chelsea ya mwisho Alhamisi ilikuwa raha tu kwa sababu mastaa wake walipania kwenda kumaliza ubishi wa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu kwenye mechi yao dhidi ya West Brom Ijumaa.
Chelsea inahitaji ushindi tu kwenye mechi hiyo kubeba taji lake la pili la Ligi Kuu England ndani ya miaka mitatu. Ushindi wa Hawthorns unawapa taji lao la tano la Ligi Kuu England. Habari njema kwao ni kuwa fiti kwa kiungo, N’Golo Kante kwenye mazoezi hayo kwa sababu Chelsea inamhitaji sana staa huyo kutimiza malengo yake.
Kocha Antonio Conte anafahamu kinachotokea hasa baada ya kikosi chake kuwa fiti mazoezini na mastaa wake wote muhimu akiwamo Kante, Eden Hazard na Diego Costa wote kuwa kwenye hali nzuri ya kuhakikisha anamaliza kabisa mbio za kusaka ubingwa huku timu ikiwa na mechi mbili mkononi.

Conte
Kabla ya mechi hiyo ya usiku, Chelsea ina pointi 84, hivyo ushindi utawafikisha katika pointi 87, ambazo hakuna timu yoyote, inayoweza kuzifikia hata kama Tottenham Hotspour inayoshika namba mbili itashinda mechi zake zote tatu zilizobaki.

Costa
Ni mafanikio makubwa kwa Kocha Conte katika msimu wake wa kwanza na kuirudisha Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya mambo kwenda kombo msimu uliopita wakati walipomaliza kwenye nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu England.

                                                   Kante
Kama itashinda mchezo huo, Chelsea itakabidhiwa kombe lake uwanjani Stamford Bridge usiku wa Jumatatu wakati itakapocheza dhidi ya Watford.

Post a Comment

 
Top