MADRID,
HISPANIA
UNATAKA
kumtumia Cristiano Ronaldo katika shughuli zako, hasa zile za matangazo ya biashara?
Inabidi uwe tajiri kwelikweli. Siri imefichuka kuhusu kiasi cha pesa ambacho
utalazimika kumlipa Ronaldo kwa nusu siku tu kwa ajili ya shughuli zako.
Waandishi
mahiri wa habari za uchunguzi za michezo, Rafael Buschmann na Michael Wulzinger
kwa kushirikiana na Mtandao wa Football Leaks unaovujisha siri mbalimbali za
mikataba ya wachezaji wamekuja na jipya kuhusu Ronaldo.
Inadaiwa
kuwa Ronaldo analipwa kiasi cha Pauni 920,000 kwa masaa manne tu ambayo
atatumia kwa ajili ya shughuli za kurekodi au kupiga picha za matangazo
mbalimbali, hii ni achilia mbali na dau halisi ya biashara hiyo.
Imebainika
kuwa mwaka 2013 Kampuni ya Saudi telecoms firm ilikubaliana na Kampuni ya
Ronaldo, Multisports & Image Management, kulipa kiasi hicho cha pesa kwa
ajili ya kuwa naye kwa saa nne na nusu na kufanya naye tangazo ambalo watu wa
Ronaldo pia katika mkataba wake halisi walitaka lionyeshwe Mashariki ya kati na
Afrika Kaskazini tu na sio dunia nzima.
Ronaldo
Kwa
mujibu wa wadaku hao, inadaiwa kuwa kampuni ya wakala wake Ronaldo, Jorge
Mendes iitwayo Gestitfute mwaka 2015 ilipiga hesabu ya utajiri wa Ronaldo na
kugundua kuwa alikuwa utajiri wa Pauni 190 milioni.
Siri
zaidi kutoka kwa wadau hao zinadai kwamba kuna mtandao mkubwa wa kampuni kutoka
katika nchi za Panama, Uswisi, Bermuda, Hong Kong na British Virgin Islands ambazo
zinamsaidia Ronaldo kutunza pesa za matangazo yake ya biashara.
Ronaldo akila bata kisiwani Ibiza
Achilia
mbali siri za Ronaldo kuvuja, Mtandao wa Football Leaks kwa kushirikiana na waandishi
hao wawili umefichua siri mbalimbali za wanasoka mahiri wa kizazi hiki wakiwemo
Mario Balotelli na kiungo aliyetimka Manchester United, Bastian Schweinsteiger.
Schweinsteiger.
Kulikuwa
na kipengele cha ajabu cha mkataba wa Balotelli na Klabu ya Liverpool
alipohamia miaka michache iliyopita kutoka AC Milan ambapo imeelezwa kuwa mchezaji
huyo alikuwa na bonasi ya Pauni 1 milioni kama angepewa kadi tatu nyekundu kwa
msimu mzima.
Kipengele
hicho kilisomeka “Kama katika kila msimu wa mkataba wake mchezaji hatatolewa
nje mara tatu au zaidi kwa kadi nyekundu kutokana na matatizo ya nidhamu kama
vile kutukana, kudharau, kutoa ishara mbaya, kuongea ovyo, basi Juni 30 ya kila
msimu mchezaji atapewa bonasi ya Pauni 1 milioni.”
Kipengele
hicho kililenga katika kumdhibiti Balotelli asifanye vituko uwanjani na
aonyeshe ubora wake ambao mara nyingi ulizibwa na vituko vya ndani na nje ya
uwanja. Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa kipengele hicho Balotelli alishindwa
kuonyesha makali yake na badala yake baada ya msimu mmoja alirudishwa Milan kwa
mkopo kisha akatolewa bure kwenda Nice ya Ufaransa katika dirisha kubwa
lililopita.
Mtandao
wa Football Leaks pia umefichua jinsi kiungo Mjerumani aliyeondoka Manchester
United katika dirisha la Januari kwenda Chicago Fire, Bastian Schweinsteiger
alivyokuwa amejipatia pesa nyingi kwa kucheza dakika chache tu uwanjani.
Balotelli
Mjerumani
huyo alikuwa akilipwa mshahara wa Pauni 7.55 milioni kwa mwaka na Manchester
United lakini alicheza kwa dakika 2,101 ambazo zilimpatia jumla ya mshahara wa
Pauni 12 milioni katika utawala wa kocha aliyepita, Louis van Gaal na kocha wa
sasa, Jose Mourinho.
Kwa
hesabu za haraka haraka, kiungo huyo alikuwa amelipwa kiasi cha Pauni 5,963 kwa
kila dakika ambayo aliichezea Manchester United licha ya kutocheza kwa
mafanikio kama ilivyokuwa wakati akiwa na Bayern Munich pamoja na timu ya Taifa
ya Ujerumani.
Post a Comment