0


IBIZA,HISPANIA
KIUNGO wa Tottenham, Dele Alli amenaswa akitanua na mpenzi wake ndani ya kisiwa na maraha cha Ibiza – baada ya matumaini ya timu yake kuchukua ubingwa kupotea.
Nyota huyo wa kimataifa wa England, 21, alionekana akimkumbatiana na mpenzi wake mwanamitindo, Ruby Mae, 22, wakiwa katika mapumziko Hispania ambapo Delle aliambatana na wachezaji wenzake Michel Vorm na Kieran Trippier.
Mastaa hao wa Spurs walikwenda kujirusha Ibiza baada ya timu yao kufungwa bao 1-0 na wapinzani wao, West Ham Ijumaa usiku.

               Dele Alli akiwa na mpenzi wake.
Mtu aliyewashudia nyota hao alisema: “Alionekana (Dele) kuwa vizuri tu.”
Hata hivyo, msimu huu ulikuwa mzuri kwa Dele baada ya kunyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Kijana wa Mwaka kwa mara ya pili.

Post a Comment

 
Top