LONDON,
ENGLAND
KIUNGO
wa Chelsea, N’Golo Kante amesema kura yake kwenye kinyang'anyiro cha Mwanasoka
Bora wa Mwaka wa England alimpigia staa wa Liverpool, Sadio Mane.
Kiungo
huyo matata mkabaji ndiye aliyeibuka kidedea kwenye tuzo hiyo akiwabwaga Eden
Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez huku
kiwango chake cha msimu huu kwenye kikosi cha Chelsea kikitajwa sababu kubwa ya
kutamba kwake.
Kante,
aliyebeba taji la Ligi Kuu England akiwa na Leicester City msimu uliopita kabla
ya mwaka huu kulikaribia taji hilo ni mmoja kati ya wachezaji wanne wa Chelsea
waliopo kwenye Kikosi cha Kwanza bora cha msimu huu.
Kante
Kante
alisema katika kinyang'anyiro cha kupiga kura alimchagua Mane licha ya kwamba
staa huyo wa Liverpool mwenye mabao 13 na asisti tano katika mechi 27
alizocheza kwenye Ligi Kuu akiwa na wababe hao wa Anfield msimu huu hakuwamo
kwenye ile sita bora iliyotinga fainali.
Kante
alizungumzia wachezaji wenzake wa Chelsea baada ya kunyakua tuzo hiyo,
"Wananipongeza kwa jambo hilo, lakini bila ya wao nisingeshinda tuzo hii.
Sadio Mane
"Tumekuwa na msimu mzuri wote kwa pamoja na nadhani tutapata kitu kikubwa zaidi kuliko hii tuzo kwa sababu soka ni mchezo wa kitimu, kama tutashinda ligi basi itakuwa vizuri kwa timu nzima kuanzia wachezaji na mashabiki."
Post a Comment