LONDON,
ENGLAND
KOCHA
Arsene Wenger ameanza kutaja orodha yake ya wachezaji anaotaka kuwasajili
katika dirisha lijalo la usajili huku likiwamo pia jina la straika kinda wa AS
Monaco, Kylian Mbappe.
Kocha
huyo wa Arsenal alisema wanamfuatilia kwa karibu fowadi huyo wa Ufaransa na
mpango wao ni kuhakikisha anatua kwenye kikosi chao mwishoni mwa msimu huu ili
kuwa na timu ya maana msimu ujao.
Lakini,
Wenger alisema shida kubwa inayowakabili na ambayo itawagharimu kwa Mbappe, 18
ni pesa kwa kuwa fowadi huyo anawindwa na timu nyingi zenye pesa hivyo
hawatakuwa na ubavu wa kushindana.
Mbappe
"Ni
wazi itakuwa ni uongo mkubwa kama tutasema kwamba hatumfutilii Mbappe,"
alisema Wenger.
"Lakini,
shida tayari ameshakuwa kwenye orodha ya klabu kibao zinazomtaka, klabu ambazo
zipo vizuri zaidi kipesa kuliko sisi."
Wenger anayesifika kwa ubahiri
Wenger
aliongeza: "Kuna klabu nyingi sana zenye pesa na zote zinamtaka. Kuna
wachezaji wachache sana wenye vipaji wanaoweza kufanya uamuzi usiozingatia pesa
kwa sasa.
“
Kwa sasa Mbappe yupo Monaco, lakini Ulaya yote wanamtaka. Siyo sisi,
tutakaomkosa, kuna wengi tu wanaomtaka watamkosa, mambo yapo kwenye pesa. Sisi
tunataka kusajili na kuwaleta hapa, tutapenda kuongeza watu."
Post a Comment