BARCELONA,
HISPANIA
SUPASTAA
wa Barcelona, Mbrazili Neymar amewaambia marafiki zake kwamba Manchester United
wapo tayari kutumia Pauni 170 milioni kuununua mkataba wake mwishoni mwa msimu
huu.
Kocha
Jose Mourinho amechenji mipango yake ya usajili baada ya straika Zlatan
Ibrahimovic kuumia goti litakalomfanya awe nje ya uwanja hadi mwakani, hivyo
sasa amelenga kutumia karibu Pauni 170 milioni kuinasa huduma ya supastaa wa
Kibrazili, Neymar.
Kwa
mujibu wa Daily Record, Neymar ameamua kuwafichulia marafiki zake wa karibu
kwamba Man United na Chelsea zinajaribu kumpima kuhusu hatima yake katika klabu
ya Barcelona.
Neymar
Kocha
Mourinho alifikia hatua ya kumwambia Neymar kwamba yupo tayari hata kumlipa
mshahara wowote anaotaka huku akinunua mkataba wa staa huyo. Oktoba mwaka jana,
Neymar alisaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuichezea Barcelona.
Mkataba
wa mchezaji huyo una kipengele kinachofichua kwamba kama kutakuwa na timu
itakayolipa Pauni 169 milioni basi itakuwa imefanikiwa kuinasa saini ya Neymar.
Masuala ya kodi yanayomwandama Neymar huko Hispania yanaweza kumfanya afikirie
kuondoka Nou Camp.
Mamlaka
ya kodi ya Hispania ilidai kwamba Barcelona haikuweka bayana ada yote ya Pauni
73 milioni iliyolipa kumsajili Neymar, ambapo Pauni 34 milioni ilikwenda kwa familia
yake. Kuhusu matumizi ya pesa kwa Man United si tatizo baada ya kumsajili Paul
Pogba kwa pesa inayoshikilia rekodi ya uhamisho kwa sasa ya Pauni 89 milioni.
Man United pia inaweza kutumia Pauni 85 milioni katika usajili wa fowadi wa
Atletico Madrid, Antoine Griezmann.
Pogba
Kocha
Mourinho bado haamini kama atamng'oa Neymar Barcelona baada ya kusema hivi:
"Licha ya kwamba Messi bado mchezaji kijana, anakaribia miaka 30, na hapo
utaona Neymar anajiandaa kuwa mchezaji mkubwa wa Barcelona baada ya Messi. Hivyo
naona ni kama kujaribu kuvunja kabati la chuma vile, haiwezekani."
Post a Comment