MANCHESTER,
ENGLAND
PEP GUARDIOLA amemtuliza Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino kwamba hana mpango wa kumchukua kiungo wake, Dele Allu.
Pamoja na hivyo Guardiola hakuacha kumsifia kiungo huyo kwamba ni
bonge la mchezaji ambaye hajawahi kutokea lakini akasisitiza kwamba hana mpango
wa kumsajil klabuni Man City msimu ujao.
Kiungo
huyo wa Tottenham amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu na ndio sababu ya
vijana hao wa Kocha Pochettino kuwa na tofauti ya pointi saba tu kati
yao na vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea.
Dele Alli
Jumanne
iliyopita Kocha Pochettino alitakaa kujihakikishia kwamba kinda huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye wiki hii
amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora Kijana wa Kulipwa (PFA) kwa mwaka wa pili
mfululizo, kama ataendelea kubaki White Hart Lane.
Lakini
pamoja na kukiri kwamba ni shabiki mkubwa wa nyota huyo wa England, Guardiola alisema
hashawishiki kumsajili katika dirisha la usajili wa majira ya joto.
“Mauricio
Pochettino anatakiwa kutulia,” alisema Guardiola. “Dele Alli ataendelea kuwa mchezaji
wake msimu ujao. Nina uhakika kuhusu hilo.
“Hatumuhitaji.
Ni mchezaji mzuri mpya katika soka la Kiingereza.
Guardiola
"Mpambanaji.
Ni mzuri. Ni mtu anayeshambulia ndani ya boski na ni kati ya wachezaji ambao
sijawahi kuwaona katika maisha yangu.
“Lakini
Manchester City haimuhitaji Dele Alli.”
City
itapambana na wapinzani wao, Manchester United, Alhamisi jioni uwanjani Etihad
katika vita ya kuwania Top Four.
Na
Guardiola amethibitisha timu yake itamkosa David Silva ingawaje inaweza
kumrudisha Gabriel Jesus katika kikosi cha kwanza.
Post a Comment