MANCHESTER, ENGLAND
HATIMAYE siri
imefichuka ndani ya Manchester United kwamba nahodha, Wayne Rooney wakati wowote anaweza kuondolewa klabuni hapo.
Hali hiyo imekuja
baada ya kufichuka kwa siri kwamba straika huyo alikuwa apigwe bei Italia katika klabu ya Napoli katika usajili
wa majira ya joto uliopita baada ya kuwa na uhusiano mbaya na Kocha, Jose
Mourinho, amefunguka wakala wa zamani
wa Fifa, Vincenzo Morabito.
Tangu kuwasili kwa
Kocha Mourinho old Trafford, Rooney amekuwa na kipindi kigumu ndani ya kikosi
cha United tangu akiambilia mabao matatu tu baada ya kucheza michezo 25 msimu
huuu.
Wakala Morabito,
aliyekuwa aki,hudumia pia mchezaji wa zamani wa Arsenal, kiungo Emmanuel Petit,
anaamini United ilijaribu kumuuza straika huyo wa kimataifa wa kabla ya siku ya mwisho ya kufungwa kwa
usajili Agosti 31.
“Ninafahamu kwa
uhakika kabisa kwamba alikuwa auzwe kwenda Napoli kwa kuwa ilikuwa ni vigumu
kumuuza katika klabu nyingine ya England,
ambayo ingeweza kumpeleka Hispania au Italia,” Morabito alifichua.
“Narudia, alikuwa atolewe
kwenda Napoli. Wazo lilikuwa zuri, kutokana na mshahara wake wa Euro10 milioni (Pauni 8.3 milioni) – kwa mwaka."
Kama vile haitoshi, Morabito
alisisitiza, kwamba mpaka sasa Rooney hatakiwi Manchester United.
“Kwa wakati huo
hakuwa na uhusiano mzuri na Mourinho, na hata hivyo hana maisha marefu United, atatolewa
hata kwa mkopo, ili kuachia nafasi,” aliongeza.
Rooney mwenye umri wa
miaka 31yuko nyuma ya mfungaji bora wa muda wote wa Manchester United, Sir
Bobby Charlton kwa bao moja akiwa na mabao 249, alianza kwa mara ya kwanza
kwenye kikosi Jumatano dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu tangu mwezi uliopita.
Post a Comment