MADRID,
HISPANIA
MKE
wa kiungo James Rodriguez, mrembo Daniela Ospina amefichua kwamba mumewe hataki
kuondoka Real Madrid na atabaki hapo kugombea namba katika kikosi cha kwanza
hadi aipate.
Hatima
ya staa huyo wa Colombia imezungumzwa sana kwa msimu huu baada ya Kocha
Zinedine Zidane kutompa nafasi mara nyingi katika kikosi chake cha kwanza.
Rodriguez ameanzishwa kwenye mechi 10 tu za La Liga msimu huu na ametokea
benchi mara nane, huku akifunga mabao matano na kuasisti mara sita.
Moja
ya mabao yake alifunga kwenye mechi ya El Clasico Jumapili iliyopita,
alipoisawazishia Real Madrid na matokeo kuwa 2-2 kabla ya Lionel Messi kufunga
katika dakika za majeruhi kuipa Barcelona ushindi wa mabao 3-2.
Hivi
karibuni, kiungo huyo ametajwa kuwa kwenye mpango wa kujiunga na Manchester
United, lakini mke wake alisema hivi: "James ametuliza akili, amekuwa na
uamuzi wake binafsi.
Rodriguez
"Ana
furaha, lakini atakapoamua kufanya uamuzi atafanya hivyo. Hawezi kuahidi kitu,
lakini kwa sasa anachotaka ni kuendelea kubaki Real Madrid na mimi napapenda
Madrid pia, nina furaha hapa Hispania na nataka nibaki. Yeye anafurahi pia na
anajaribu kupambana kupata nafasi, mimi nataka acheze kila siku, hapo siwezi
kudanganya.
Rodruguez akiwa na mkewe
" Rodriguez amekuwa mchezaji wa Real Madrid tangu mwaka 2014
alipojiunga akitokea Monaco baada ya kuonyesha kiwango kikubwa sana kwenye
Kombe la Dunia akiwa na Colombia.
Post a Comment