MANCHESTER,
ENGLAND
SUPASTAA
Zlatan Ibrahimovic amegoma kupokea ofa ya kulipwa Pauni 13 milioni kutoka
Manchester United kwa kusema hawezi kupokea pesa ambayo haifanyii kazi.
Kocha
Jose Mourinho alimwambia Zlatan kwamba anataka kumwongeza mwaka mmoja kwenye
mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo licha ya kwamba amepata majeraha ya
goti yanayomweka nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi tisa, lakini mwenyewe
amekataa kupokea ofa hiyo. Ibra aliona si jambo zuri kukubali kulipwa pesa
wakati hachezi.
Ibrahimovic
Kwa
maana hiyo, Ibra atakuwa amehitimisha rasmi maisha yake ya huko Old Trafford
baada ya kuumia goti katika mechi ya Europa League dhidi ya Anderlecht.
Majerahi hayo yatamlazimu kufanyiwa upasuaji ambao utamfanya awe nje ya uwanja
kwa muda mrefu na ataonekana uwanjani tena kuanzia mwakani.
Wakati
Man United ilipomsajili Ibra mwaka jana ilimsainisha mkataba wa mwaka mmoja
wenye thamani ya Pauni 250,000 kwa wiki na kulikuwa na uwezekano wa kuongeza
mwaka mmoja zaidi kama pande hizo mbili zitakuwa zimefikia makubaliano.
Katika msimu wake wa kwanza Old Trafford, Ibra
amefunga mabao 28 na ndiyo maana Man United ilihitaji abaki kabla ya majeruhi
kuja kutibua.
Post a Comment