0


KIVUMBI cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kimefika patamu baada ratiba ya hatua ya 16 Bora kutoka.
Baada ya maneno mengi, hatimaye imebainika Arsenal imepangwa kucheza dhidi ya Bayern Munich, wakati Barcelona itakipiga dhidi ya Paris Saint-Germain.
Mabingwa watetezi, Real Madrid watapepetana na Napoli na Manchester City itakutana na Monaco.
Arsenal, ambayo ilishika nafasi ya kwanza katika kundi lake kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2011-12, itataka kushinda ili kufikia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2009-10.

Beki Per Martesacker wa Arsenal akisikitika huku wachezaji wa Bayern wakifurahi baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Arsenal.
Miamba hiyo ya England inayofahamika kama ‘The Gunners’ inakutana na Bayern baada ya kucheza nayo katika hatua ya makundi mwaka jana na kutolewa pia ilitolewa katika hatua ya -16 na Wajerumani hao 2012-13 na 2013-14.
PSG, ilishinda dhidi ya Barca ilipokutana nayo kwa mara ya kwanza katika hatua ya robo fainali 1994-95, lakini  Wacatalunya hao walishinda walipokutana robo fainali misimu ya 2012-13 na 2014-15.

Wachezaji wa Bayern wakijipongeza baada ya ushindi wa mabao 2-0 uwanjani Emirates dhidi ya Arsenal mwaka 2014.
Klabu hizo pia zilikutana katika hatua za makundi mwaka 2014, ambapo PSG ilishinda uwanjani kwake Parc des Princes na Barca ikashinda Camp Nou.
Mkurugenzi wa michezo wa PSG, Patrick Kluivert, ambaye ni straika wa zamani wa Barcelona, alisema: " Unajua matarajio ni kupangwa na timu moja kubwa ya dunia.
"Tuna uzoefu wa kucheza dhidi ya Barcelona kwa mara kadhaa katika robo fainali na mara moja katika hatua ya makundi.

Arsene Wenger akimdhahaki Arjen Robben wa Bayern.
"Tunapaswa kukabiliana nao. Hiyo ni ni ratiba. Hatuwezi kuificha."
Makamu Rais wa Barca, Jordi Mestre: "(PSG) siyo timu rahisi kucheza nayo. Hadi sasa mambo yamekwenda vizuri tangu tulipocheza nayo, lakini kila msimu ni tofauti. Katika Ligi ya Mabingwa hakuna timu nyepesi. Nje ya ratiba hiyo, Bayern ilikuwa timu ngumu zaidi, lakini PSG ni timu kubwa."

Straika wa Barca, Lionel Messi akishangilia bao.
Real Madrid itacheza dhidi ya Napoli ikijipanga kuwa timu ya kwanza kushinda taji hilo mfululizo kwa mara ya kwanza. Kikosi hicho cha Kocha Zinedine Zidane kimesimama kileleni katika Ligi ya la Liga kikiwa na tofauti ya pointi sita na kikiwa na rekodi ya kutofungwa katika michezo 35.
Kikosi cha Pep Guardiola cha Manchester City, kilichofika nusu fainali katika mashindano ya msimu uliopita, kimepangwa dhidi ya Monaco.

Manchester City msimu uliopita ilifika nusu fainali.
Kocha Guardiola ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa mara mbili akiwa na Barca, na amefika nusu fainali mara tatu mfululizo alipokuwa akiifundisha Bayern.
Mkurugenzi wa soka wa Man City, Txiki Begiristain alisema: "Ni vigumu kusema ratiba ni ngumu au rahisi. Tunafurahi kufikia hapa.
"Monaco inafanya vizuri, ina wachezaji wazuri, vipaji vizuri, wachezaji vijana na wanacheza soka zuri Ufaransa.
"Bila shaka kwa mara kadhaa katika hatua hii tumekuwa tukicheza dhidi ya  Barca. Real na Bayern Munich. Ni jambo zuri kuziepuka."

Leicester City kwa mara ya kwanza imefika hatua ya mtoano.
Washindi wa pili  wa msimu uliopita, Atletico Madrid, itacheza dhidi ya Wajerumani, Bayer Leverkusen, wakati Juventus itakumbana na Porto.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu  England, Leicester City itacheza dhidi ya Mabingwa wa Europa Sevilla baada ya kushika nafasi ya kwanza kwenye kundi lao, na Miamba ya Ureno, Benfica itacheza na Borussia Dortmund.
Michezo ya kwanza itapigwa kati ya Februari. 14, 15, 21 na 22 na michezo ya marudiano itapigwa Machi 7, 8, 14 na 15.
RATIBA KAMILI
Manchester City
v
Monaco
Real Madrid
v
Napoli
Benfica
v
Borussia Dortmund
Bayern Munich
v
Arsenal
Porto
v
Juventus
Bayer Leverkusen
v
Atletico Madrid
Paris Saint-Germain
v
Barcelona
Sevilla
v
Leicester C

Post a Comment

 
Top