0


MILAN, ITALIA
SAMUEL ETO’O  ameonekana kutojali taarifa za kuweza kuhukimiwa kunyongwa au kufungwa miaka 10 na nusu jela,  na ndio kwanza ameonekana akifurahia maisha jijini Milan, Italia akiwa katika mashindano ya urembo.
Kwa mujibu wa wanasheria wa Hispania, straika huyo wa zamani wa Chelsea na Barcelona anatakiwa kufikishwa mahakani kwa kukwepa kodi na mamlaka za kodi za Hispania
Kwa mujibu wa Gazeti la El Pais, Eto’o alijipatia kinyume cha sheria Pauni 3 milioni kuanzia mwaka 2006 hadi 2009, wakati akiwa Nou Camp.
Hata hivyo, pamoja na taarifa hizo nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Cameroon amenaswa akiwa amejawa na tabasamu jijini Milan sambamba na mkewe Georgette.
 Akiwa  amevaa skafu, kofia na saa ya dhahabu, Eto’o na mkewe walionekana kujawa na vicheko.
Pamoja  na kifungo hicho cha muda mrefu jela, waendesha mashtaka wanataka apigwe faina inayokadiriwa kufikiwa Pauni 12 milioni.
Eto’o anatumiwa kukwepa kodi kutokana na sheria ngumu iliyowekwa  Hispania ya haki ya kumiliki picha.
Straika huyo alikuwa akiendesha  makampuni mawili Bulte 2002 nchini Hispania na Tradesport nchini Hungary- na kuweza kuhamisha haki ya picha zake kati ya makampuni hayo na kukwepa kulipa kodi.
Wakati huohuo, waendesha mashtaka hao wa Hispania  wanataka mshambuliaji wa sasa wa Barcelona,Neymar afungwe jela miaka mitano.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 24, anatuhumiwa kuhusika katika udanganyifu wa uhamisho wake kutoka Klabu ya Santos na kujiunga na Barcelona mwaka 2013.
Eto'o aliichezea Barcelona michezo 198 kati ya mwaka 2004  hadi 2009, alifunga mabao129. 

Alibeba taji la Ligi ya Mabingwa mara mbili alipokuwa Nou Camp  na alikusanya medali tatu za La Liga kabla ya kutimikia Inter Milan.

Pia, fowadi huyo alicheza Ligi Kuu ya England kwa kuzitumikia Chelsea na Everton.  

Julai mwaka huu, straika wa Barcelona, Lionel Messi na baba yake walihukumiwa kifungo cha miezi 21jela kutokana na ukwepaji kodi, ingawaje hajafungwa jela kutokana na sheria za Hispania kosa la kwanza likiwa chini ya miaka miwili linaweza kuarishwa.

Post a Comment

 
Top