MANCHESTER,
ENGLAND
YAYA
TOURE ametoa taarifa ya wazi kumuomba radhi bosi wake, Pep Guardiola na klabu
yake ya Manchester City akionekana anataka kurudi uwanjani Etihad. Kiungo huyo Muivory Coast hajacheza mchezo wowote chini ya Guardiola tangu ule wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Steaua Bucharest uliochezwa Agosti.
Bila ya uwepo wake, Guardiola ameiongoza City kileleni mwa Ligi Kuu England- na Jumanne usiku iliifunga timu ya zamani ya Toure, Barcelona mabao 3-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wiki iliyopita, Guardiola alionyesha dalili za kutaka kumchagua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Manchester United kama angeombwa msamaha na wakala wa Toure, Dimitri Seluk.
Na Toure aliachia taarifa yake ya kuomba radhi Ijumaa ili kuweka mambo sawa na kuondoa kutokuelewana na kocha wake huyo.
Kazi yangu ni kucheza soka.
“Ninapenda
kuomba msamaha – kwa niaba yangu mwenyewe na wote wanaoniwakilisha– kwa utawala
wa timu na wote wanaoitumikia klabu kutokana na kutokuelewana kulikotokea siku
za nyuma,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo. “Taarifa zote hazikuwakilisha mawazo yangu juu ya klabu au watu wanaofanya kazi hapo. Sina kitu lakini heshima kwa Manchester City na kuitakia mafanikio klabu.
Pep Guardiola na Seluk.
“Binafsi
ninajivunia kuwa sehemu ya historia ya klabu na ninataka kuisaidia City kupata
mafanikio zaidi. Napenda kucheza soka na kuwapa furaha mashabiki.“Kwa taarifa hii, napenda kuwashukuru mashabiki kwa ujumbe wao katika kipindi hiki kigumu. Hii ina maana kubwa kwangu na familia yangu.”
Habari zilizopatikana Alhamisi jioni zinasema Yaya Toure alimwambia wakala wake kufanya maelewano na Guardiola.
Siku za hivi karibuni kulikuwa na vita vya maneno kati ya wakala wa mchezaji huyo, Seluk na bosi wa Manchester City Guardiola.
Shabiki mtoto akitaka Yaya achezeshwe.
Wakala
huyo alimtuhumu Guardiola kumnyanyasa mteja wake na kocha huyo alichukua uamuzi
wa kumweka benchi Yaya hadi atakapoombwa radhi. Katika mazungumzo yake ya Ijumaa, Seluk amekiri kuambiwa na Yaya Toure kufungua ukurasa mpya na Guardiola kwa matumaini kwamba kiungo huyo atarudishwa kikosini City.
Post a Comment