0


INSTANBUL, UTURUKI
PAUL SCHOLES anaamini itachukua miaka mingine miwili kwa Kocha, Jose Mourinho kutengeneza kikosi kinachoweza kutoa changamoto na kutwaa mataji. 
United ikiwa na kikosi cha gharama imekatisha tamaa baada ya kufungwa mabao 2-1 Alhamisi dhidi ya Fenerbahce katika Europe League.
Mashetani Wekundu hao, sasa wana wasiwasi mkubwa wa kukosa kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo, pamoja na kutumia Pauni145 milioni katika usajili wa majira ya joto.
Na Scholes anatarajia kuona mabadiliko baada ya miaka misimu miwili ijayo.
“Imenitia uchungu kwa miaka mitatu na nadhani inahitaji miezi 18 mingine au miaka miwili hadi kocha atakapofanya usajili katika madirisha matatu au manne ndio anaweza kupata timu anayoitaka,” alisema Scholes.

Itachukua misimu miwili kukaa sawa.
“Nadhani ni miaka miwili, hii timu itakaa sawa kwa kile tunachokifanya sasa lakini vinginevyo itakuwa ni ziada tu. 
“Wanaweza kushinda League Cup, Wanaweza kushinda Kombe la FA Cup. Wanaweza kushinda mashindano haya? 
“Haionekani kama inaweza na wameonyesha katika miaka mitatu kwamba hawana uwezo wa kushinda Ligi Kuu na kikosi hiki.”

Maji yalipozidi unga uwanjani.
Tayari Kocha Mourinho ameanza kukumbana na mlima wa presha ndani ya miezi mitano ya utawala wake Old Trafford. 
Mashetani Wekundu hao wameshinda michezo miwili tu kati ya michezo saba ya mwisho katika mashindano yote na tayari iko nyuma kwaa pointi nane nyuma ya vinara wa Ligi Kuu wapinzani wao wa jadi Manchester City.

Mashabiki wataka Mourinho aondoke.
Kama vile haitoshi, Mourinho anaingia changamoto ya kumkosa kiungo wake aliyevunja rekodi ya dunia Mfaransa, Paul Pogba, baada ya kuumia katika nusu ya kipindi cha kwanza katika mchezo huo dhidi ya Fenerbahce jijini Istanbul.

Pogba akichechemea.
Kocha huyo Mreno anatarajia matokeo chanya Jumapili hii pindi timu yake itakaposafiri kwenda Swansea katika mchezo wa Ligi Kuu.

Post a Comment

 
Top