0


LISBON, URENO
NI vigumu kuamini lakini ndivyo ilivyo. Straika wa kimataifa wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo pamoja na kufanya kila kwa faida ya nchi yake bado amekuwa sawa na nabii asiyekubalika kwao.
Hayo yamebainishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Paulo Futre aliyesema Ronaldo hapendwi na watu wote nchini kwake, kwani baadhi ya watu wa Ureno wanatarajia Lionel Messi atashinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia, 2016 Ballon d'Or.
"Cristiano (Ronaldo) ni Mreno, amefanya kila kitu, ikiwamo ubingwa wa Ulaya," alisema Futre. "Lakini ana maadui wengi pale- kutokana na jinsi alivyo. Yuko muwazi, na kumfanya atengeneze maadui katika nchi yake.
"Kuna wakati mwingine watu wengi wanaimba 'Messi, Messi, Messi' nje ya hoteli ya timu ya taifa ya Ureno. Kitu ambacho ni aibu. Bila shaka kuna watu wa Ureno wanaotaka Messi ashinde Ballon d'Or."

Futre alisema baadhi ya watu wana matatizo na Ronaldo kwa jinsi anavyojiweka ndani na nje ya uwanja.
Hata hivyo, mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid, kwa binafsi yake alisema hakufurahishwa na jinsi Ronaldo alivyoshangilia  mabao ya Real Madrid katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Altletico Madrid uwanjani Estadio Vicente Calderon Jumamosi iliyopita.
"Maneno anayosema wakati mwingine baada ya mechi, na tabia yake..." Futre alisema. "Kwa  kile alichofanya Calderon- alitakiwa kuwa na utulivu, lakini tumemuona Cristiano yukoje. Ana uzoefu wa kutosha katika hatua hii.

"Kadiri anapopondwa katika viwanja mbalimbali vya ugenini, ndivyo anavyopata hamasa. Lakini bila shaka ana miaka 31 sasa. Nafahamu ilikuwa derbi na siku zote ina joto kali zaidi. Binafsi yangu nimesikia mengi pindi anapokwenda katika viwanja vya ugenini, lakini kuwa Mreno."
Futre alisema angekuwa na wakati mgumu kuchagua kati ya Ronaldo na nyota wa kimataifa wa Ufaransa na Atletic Antoine Griezmann  kwa ajili ya Ballon d'Or.
"Baada ya msimu (Griezmann) alistahili bila ya wasiwasi," alisema. " Lakini  baadaye Cristiano pia, naamini atakuwa mmoja kati yao.

“Ninaamini kwamba Messi, mwaka huu, yuko nyuma ya wawili hao. Kwa miaka kadhaa sasa, inategemea na muda nani ni bora kati ya Messi  na Cristiano.
Jumanne iliyopita Ronaldo akiwa na Real Madrid alikuwa Ureno kucheza dhidi ya timu yake ya zamani ya Sporting Lisbon katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 uwanjani Estadio Jose Alvalade.

Post a Comment

 
Top