0


MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO amethibitishwa kwamba Manchester United itaongeza mkataba na straika wake, Zlatan Ibrahimovic kwa msimu wa pili.
Ibrahimovic, 35, alijiunga na United bure akitokea Paris Saint-Germain katika usajili wa majira ya joto na wiki alisema anafikiria kucheza soka katika Ligi ya Marekani kwa siku za baadaye. Mpaka sasa straika huyo ameifungia Uniyed mabao manane  na anapata mshahara wa Pauni 260,000 kwa wiki.
"Suala la Zlatan ni rahisi mno," Mourinho aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano kuelekea mchezo wa Alhamisi dhidi ya Feyenoord.
"Yeye ni sawa na moja jumlisha moja. Tuna furaha kuwa naye. Tunakwenda kutekeleza fursa kwa msimu wa pili. Baada ya hapo atafanya anachotaka."

“Kwa hiyo ndani ya miaka miwili  anaweza kufanya anachotaka kwa sababu yuko huru. Miezi 18 atakuwa na furaha, amejifunga, anayapenda kama mchezi wa soka wa United – mwishoni ni changamoto kubwa katika kazi yake.
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Sweden alikuwapo kwenye mkutano huyo na alipoulizwa, kuhusu kuongeza mkataba,alisema: " Kwa sasa, hatujajidiliana. Nina mkataba unaosema mmoja (mwaka) jumlisha moja.

"Ninajisikia vizuri, niko safi, ninajiona niko kwenye kiwango, kwa hiyo bila shaka kutakuwa mwaka wa pili. 
"Ninataka kufanya kile ninachoweza kufanya na sio kupoteza muda. Mwaka wa pili unakwenda baada wa kwanza, kama utaendelea kama hivi, sawa."

Post a Comment

 
Top