0


MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO amekalia kuti kavubaada ya baadhi ya mashabiki kuanza kumshambulia na kumtaka atimuliwe.
Mashabiki wenye hasira walitumia mitandao ya kijamii kuonyesha hasira zao juu ya kocha huyo.
Hali hiyo inajitokeza baada ya kipigo cha Alhamisi cha mabao 2-1 dhidi ya Fenerbahce katika Europe League na kumfanya Mreno huyo kuwa na mwanzo mbaya wa msimu kuliko makocha wengine waliokuja baada ya kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, Manchester United- wakiwamo, David Moyes na Louis van Gaal.
Kipigo hicho cha Fenerbahce kimeendeleza matatizo ya United tangu alipoondoka Ferguson mwaka 2013.
Mpaka sasa, Mourinho ameshinda michezo minane, amepata sare tatu na amepoteza michezo mitano kati ya michezo16 tangu aanze kibarua hicho United.
Hii ni tofauti na Van Gaal, ambaye ameshinda michezo minane, sare nne na amefungwa mechi nne, wakati Moyes, ameshinda mechi tisa, sare tatu na amefungwa michezo mitatu.

Mourinho akitafakari.
Mbali na kipigo alichokipata Uturuki Alhamisi, vipigo vingine vya Mourinho vilikuwa katika Ligi Kuu England dhidi ya Manchester City, Watford na Chelsea- ukijumlisha na ule wa Europa League dhidi ya Feyenoord.

Van Gaal aliondolewa
Kocha Van Gaal vipigo vyake vya mapema vilikuwa ni dhidi ya Swansea City, Leicester City na Manchester City- na katika Kombe la Ligi dhidi ya Milton Keynes Dons.

Moyes hali naye ilikuwa mbaya.
Kwa upande wake, Moyes alifungwa katika Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool, Manchester City na West Bromwich Albion.

Post a Comment

 
Top