BARCELONA, HISPANIA
NEYMAR huenda
akatumikia jela miaka miwili baada ya usajili wake wa mwaka 2013 kujiunga na
Barcelona kugubikwa na sakata la rushwa.
Hayo ni mapendekezo
yaliyotolewa na wanasheria wa serikali ya Hispania katika kesi inayomkabiri
staa huyo na baba yake pamoja na rais wa klabu ya Barcelona wa zamani, Sandro
Rosell.
Pia, waendesha
mashataka hao wamemtaka Jaji, Jose Perals kumuhukumu, Rosell kifungo cha miaka
mitano na kutozwa faini ya Euro 8.4 million (Pauni 7.2 milioni) kwa klabu hiyo.
Katika hatua nyingine
wanasheria hao wameitaka mahakama hiyo kumfutia mashtaka rais wa sasa wa
Barcelona, Josep Maria Bartomeu.
Rais Rosell, Neymar na
baba mzazi wa nyota huyo wa kimataifa wa Brazili wanatakiwa kujitetea dhidi ya
mashataka hayo.
Msingi wa kesi hiyo
umetokana na malalamiko ya Kampuni ya Uwekezaji ya Kibrazili (DIS), ambayo
inamiliki asilimia 40 ya haki ya uhamisho wa Neymar na ilidai kupokea kiasi
kichache zaidi ya uhamisho halisi wa straika huyo.
Rais Rosell alijiuzulu
nafasi yake hiyo mwaka 2014 na alitoa ushihidi wake mahakamani Februari
sambamba na Bartomeu, Neymar na baba wa staa huyo.
Barca ilifanikiwa
kutenganisha kesi hiyo Juni na kulipa faini Pauni 4.7 milioni na kukwepa
mashtaka ya ukwepaji kodi katika uhamisho.
Hata hivyo, pamoja na
Jaji, Jose de la Mata kukubaliana na Barca mwezi Juni, waendesha mashataka hao
wa serikali wamefanikiwa kuirudisha tena kesi hiyo tena mahakamani na kutaka
klabu hiyo ihukumiwe upya.
Straika mwenza wa
Neymar ndani ya kikosi cha Barcelona,
Lionel Messi alihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa kosa la ukwepaji kodi
mapema mwaka huu.
Messi alikata rufaa
dhidi ya kifungo na katika mfumo wa sheria za Hispania kifungo chini ya miaka
miwili kinaweza kuahirishwa.
Tangu amejiunga na
klabu hiyo ya Nou Camp, Neymar mwenye umri wa miaka 24- ameshinda mataji mawili
ya Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, mawili
ya Copa del Rey, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europe Super Cup, Hispania Super Cup
na Kombe la Dunia la Klabu.
Neymar amesaini
mkataba wa miaka mitano na Barcelona mwezi Oktoba.
Post a Comment