MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO ametetea uamuzi wake
wa kumrudisha kiungo, Bastian Schweinsteiger katika kikosi cha kwanzaa cha Manchester
United na kusema ni uamuzi wa kitaamu zaidi.Kocha Mourinho alisema nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani alifanya vizuri alipokuwa nje ya kikosi hicho na alitumika pindi palipokuwa na tatizo katika nafasi ya kiungo.
Jumatatu, United iliachia picha zinazomuonyesha Schweinsteiger na Henrikh Mkhitaryan wakiwa mazoezini.
Kiungo, Schweinsteiger alisajiliwa na Kocha Louis van Gaal mwaka 2015 aliatemwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza kufutia kuwasili kwa Mourinho katika majira ya joto.
Kiungo huyo alisema atakuwa tayari kuondoka Agosti pindi ikitokeaa timu inayomhitaji lakini United ilimfananisha mchezaji huyo na rasilimali ya klabu.
Schweinsteiger mazoezini
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32
alijumlishwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa Ligi Kuu lakini hajajumuishwa
katika Europa League, ikimaanisha kwamba hataweza kucheza katika michuano ya
Ulaya hadi mashindano hayo yatakapofikia katika hatua ya mtoano.
Schweinsteiger akitaniana na wenzake
Hata hivyo imebainika kwamba,
kurudishwa kwake kumetokana na Ander Herrera-mwenye jukumu la kucheza kwenye
nafasi kuonyeshwa kadi nyekundu Jumamosi katika mchezo dhidi ya Burnley
ulioisha kwa sare ya 0-0.Kiungo Schweinsteiger hakuonyesha dalili za upinzani kuhusu kuwekwa kwake nje ya kikosi, akituma ujembe chanya katika akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Na akizungumza katika mkutano Jumatano, Mourinho alisema: "Schweinsteiger amerudi.
"Tulifanya uamuzi huo Alhamisi iliyopita. Tulimpigia simu Ijumaa iliyopita anaweza kuungana na timu Jumatatu.
"Ni uamuzi ambao unaendana na ukweli kwamba tupo katika kipindi cha msimu mgumu ambao unahitaji unatuhitaji kuwa pamoja na kila mtu.
Schweinsteiger akipasha misuli
"Ukimwangalia Bastian na jinsi
alivyofanya kazi kila siku na makocha wazuri, tunadhani tumefanya uamuzi wa
kitaalamu kumrudisha kwenye timu."Tutajiandaa vizuri na kuwa katiak hali nzuri- labda katikan uamuzi wake wa baadaye wa kuondoka klabuni.
"Kwa sasa hatuna matatizo katika nafasi ya kiungo, kama tulivyo kwenye ulinzi. Kama tutakuwa na matatizo katika kiungo, yeye ni suluhisho letu."
Kocha Mourinho.
Wachezaji wanne wa safu ya ulinzi ya
United imekumbwa na majeraha - Antonio Valencia, Eric Bailly, Chris Smalling na
Phil Jones na kuukosa mchezo wa Burnley.Beki Marcos Rojo na Matteo Darmian walianza kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu msimu huu, lakini Phil Jones amerudi mazoezini na ametajwa katika kikosi cha wachezaji 21- katika mchezo wa Alhamisi wa Europa League dhidi ya Fenerbahce.
Post a Comment