BARCELONA, HISPANIA.
BARCELONA imefungua
mazungumzo ya mkataba na Luis Suarez na inaamini straika huyo atasaini dili la
mkataba mpya pamoja na kuahidiwa dau la uhamisho litakalovunja rekodi ya dunia
na Manchester United.
Ripoti ya wiki
iliyopita ilisema Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho yuko tayari kutumia
Pauni 135 milioni kumpeleka nyota huyo wa zamani wa Liverpool, Old Trafford baada
ya kuchanganywa na uhaba wa mabao katika kikosi chake.
Lakini Rais wa Barca,
Jose Luis Bartomeu ameweka wazi kwamba tayari miamba hiyo ya Catalunya iko
katika mazungumzo na wawakilishi wa Suarez kuhusu kumuongezea mkataba mpya, kutokana
na huu wa sasa kutarajiwa kumalizika msimu wa majira ya joto 2019.
Suarez akiitumikia Barca dhidi ya Man City.
Akizungumza kuhusu
tetesi zinazomuhusu nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 29
kwenda Manchester United, Bartomeu alisema: “Tumesoma, tumesikia, tumeziona
habari, lakini bila shaka, matumaini yetu katika suala hilo ni kwamba Suarez anafurahia
maisha ya Barcelona.
“Kwangu binafsi, bila
shaka ni straika bora Ulaya na tunataka kubaki naye.
Suarez
“Tunajaribu kuongeza
mkataba wake na Barcelona na ni mmoja kati ya matarajio yetu ya baadaye kwa
sababu bado kijana, ana mtazamo wake na matumaini kibao.
“Anafuraha Barcelona
na pamoja na Lionel Messi na Neymar, kwa kweli safu yao ni hatari sana.”
Hivi karibuni Barcelona
iliwapa mikataba mipya, Neymar na beki Javier Mascherano, wakati ikipanga kufanya
mazungumzo ya mkataba mpya na Messi mwezi ujao.
Bosi wa Manchester
City, Pep Guardiola hivi karibuni alikaririwa jinsi anavyomzikia Messi na
kumkaribisha mchezaji huyo Etihad kama atahitaji kuondoka Barcelona na kutaka
kukabiliana na changamoto mpya.
Mourinho anatishwa na washambuliaji wake.
Alipoulizwa
kama mpanga huo una uhusiana na Man City kutaka kumnasa Messi, Bartomeu alisema:
'Hapana, siwezi kudanganya. Huu ni uamuzi wa Messi au kwa mchezaji yeyote
anayetaka kubadili klabu.
“Mpaka sasa Messi ana
mkataba nasi utakaokwisha wakati wa fainali za Kombe la Dunia (2018) na
tunafurahi kuwa naye. Ni mchezaji bora wa dunia hadi sasa.”
Post a Comment