BARCELONA, HISPANIA
NI Msaidizi
wa Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, Mikel Arteta ndiye aliyempandisha mori Lionel
Messi na kufamfanya straika huyo kuropoka maneno ya hasira uwanjani Etihad Jumanne usiku, kwa mujibu wa
Radio ya Hispania, La Cope.
Kituo hicho
kimeripoti kwamba wakati Messi akisubiri nje ya vyumba vya waamuzi, Arteta
alisema: 'Anda tontorrón, vete y métete en tu vestuario,' akimaanisha: “Ondoka
mpumbavu, nenda kwenye vyumba vyenu vya kubadilishia nguo.'
Messi aliyekuwa
amechanganyikiwa baada ya Barcelona kufungwa katika hatua ya makundi ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya ikiwa na mara ya kwanza ndani ya miaka miwili alijibu, kwa kupiga
kelele: Bobo, vení y da la cara!', a sort of) akimaanisha :“Njoo useme maneno
yako mbele yangu, mpumbavu.”
Messi
Vita kama hiyo iliwahi
kutokea mwaka Oktoba 2004 kati ya wachezaji wa Arsenal na Manchester United
chini ya handaki.
Kocha Msaidizi
alikuwa kama Cesc Fabregas katika tukio hilo ingawaje lilimjumuisha pia Fernandinho
na baadhi ya wafanyakazi wenye hadhi
ndogo kwenye vyumba vya Manchester City.
Hata hivyo, Fernandinho
haraka alikanusha tetesi za kuhusika katika mazingira ya tukio hilo, akijiweka
mbali kupitia mindano ya kijamii.
Arteta akiwa na benchi la ufundi.
“Nataka kusema minong’ono
inayozunguka katika vyombo vya habari ni ujinga: Sijawasiliana hata na mchezaji
yeyote wa Barcelona au benchi la ufundi baada ya mchezo,” alituma katika
mtandao wake wa Twitter.
“Kuchochea na kuudhi
siyo asili yangu, akilini mwangu najua umuhimu wa kuonyesha heshima kote ndani na
nje ya uwanja, bila ya kujali au kumhoji mchezaji wa upinzani.”
Imebainika kwamba majibu
ya Messi yalikuwa yanamlenga mtu maarufu na anayezungumza Lugha ya Kihispania
kwa ufasaha.
Messi akiwa kazini.
Messi alitulizwa na staa
mwenzake wa timu ya taifa ya Argentina, Sergio Aguero baada ya kufunga bao lake
la saba katika michezo mitatu ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu huu.
Staa huyo wa
Barcelona amefunga mabao 54 katika hatua ya makundi na kuweka rekodi mpya na kuipita ile ya Raul ya mabao 53.
Straia Aguero alisema
lilikuwa ni tukio lililozuka ghafla na
alifanya jukumu lake.
“Unapopoteza unakuwa
hauna furaha,” alisema fowadi huyo wa City.
Arteta atajwa kumpandisha mori Messi.
“Nilimuona (Messi)
pale, alikuwa akijisikia vibaya. Namjua kiasi fulani anapokuwa katika hali
mbaya na anapokuwa vizuri. Lakini unapopoteza mchezo, hakuna uzuri.
Aguero na Messi.
“Nilidhani Messi angesema
neno kwangu lakini hakufanya hivyo, na tukazungumza mambo mengine. Haikuwa jambo
makini. Nilisikia kitu faulani lakini
sikujua nini kimetokea.
Post a Comment