MANCHESTER,
ENGLAND
WAYNE ROONEY
amekiri kwamba alistahili kukaa benchi katika klabu yake ya Manchester United lakini
amesisitiza hajakwisha kiasi cha kutokuwav na guvu za kuitumikia klabu hiyo na
timu yake ya taifa.
Nahodha huyo
wa England amewekwa benchi katika michezo mitatu ya mwisho ya United, baada ya
kucheza vibaya dhidi ya Watford Septemba 18, na kuwafanya wakosoaji wake kudai
kwamba huenda ukawa ndio mwisho wa mchezaji huyo.
Straika huyo
yuko katika wakati mgumu baada ya kuwa katika kiwango kizuri miaka yake14- na
amekiri uwanjani St George's Park kwamba hana kasi kama alivyokuwa lakini
akaahidi atafanya kitu cha kuwashawishi kocha wa United, Jose Mourinho na yule
wa muda wa England, Gareth Southgate kumtegemea.
“Watu wana
maoni yao na ni haki kuyasikia,” alisema Rooney ambaye hajui kama Southgate atamwanzisha
katika mchezo dhidi ya Malta Jumamosi.
Rooney akiwa benchi.
“Ni mchezo
wa soka huwezi kucheza kwa muda wote hata kama utataka. Niko katika hatua ninayotaka
kucheza. Mimi ni mpiganaji. Nataka kurudi katika timu.
“Nitapambana kwa
nguvu zangu zote kujaribu kulifanya hilo. Katika kipindi hiki nimekosolewa sana.
Hapa ndipo nilipo. Nina uhakika watu wanaonijua wanajua nitarudi. Nimecheza
vibaya, nafahamu na nalitambua hilo. Nadhani kama angechagua kikosi kingine
nyuma ya hicho nafahamu nisingecheza.
Rooney akiri kwamba
tangu mchezo dhidi ya Leicester timu imefanya vizuri. Na anajua kama anatakiwa
kupambana kuweza kurudisha nafasi yake.
Rooney, ana matumaini ya kuendelea
kuitumikia England ili kuweza kuvunja rekodi
ya Peter Shilton ya kucheza michezo 125.
Post a Comment