MANCHESTER, ENGLAND
PEP GUARDIOLA hataki
masihala kabisa akiwa katika kazi yake. Sasa amepiga marufuku matumizi ya
internet klabuni Manchester City.
Guardiola
ameruhusu maeneo machache ya eneo la kisasa la mazoezi la Manchester City, The
City Football Academy kupata internet lakini amepiga marufuku na kukata mawasiliamo
katika maeneo ya ndani kwa ajili ya kuwataka wachezaji wake wazingatie zaidi
mazoezi yake.
Beki
wa kimataifa wa Argentina, Pablo Zabaleta amedai kwamba Guardiola ameamua
kuyafanya maisha yao kuwa magumu katika matumizi ya simu au vifaa vinginevyo
vinavyotumia Internet kwa ajili ya kuwafanya wazingatie zaidi anachowafundisha.
“Anatulazimisha
kula chakula cha asubuhi na cha mchana pamoja klabuni. Internet imekatwa na
tunakaa bila ya mawasiliano na watu wa nje. Hatuwezi kutumia 3G,” alisema beki huyo
wa kimataifa wa Argentina ambaye ameendelea kupata namba chini ya Guardiola.
Zabaleta,
ambaye alinunuliwa na City mwaka 2008 akitokea Espanyol ya Hispania hata hivyo
amedai kwamba anafurahishwa na mbinu za kocha huyo wa zamani wa Barcelona na
Bayern Munich aliyetua klabuni hapo msimu huu.
“Siku
zote unaota ndoto za kufanya mazoezi chini ya makocha bora na leo nimepata
nafasi ya kufanya kazi na mmoja kati ya makocha bora. Kwa kweli unajifunza
sana, sana sana jinsi ya kuishi. Zaidi ya ufahamu wake wa soka lakini pia
mapenzi yake kwa soka,” aliongeza Zabaleta.
Hii
ni mara ya pili kwa Guardiola kuonyesha makali yake katika kambi ya mazoezi ya
City. Julai mwaka huu wakati City wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu
beki wa kushoto wa timu hiyo, Gael Clichy alidai kwamba Guardiola alikuwa
amepiga marufuku baadhi ya vyakula.
Zabaleta
“Uwanjani
na nje ya uwanja kila kitu kinaangaliwa kwa umakini. Kwa mfano, utawasikia
makocha wakisema kwamba afya ni muhimu. Kwa Guardiola, kama uzito wako ni
mkubwa basi haufanyi mazoezi na kikosi cha kwanza.
“Ni
kitu ambacho unakisikia sana lakini kwangu ni mara ya kwanza kwa kocha kufanya
hivyo. Kwa hiyo kuna wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza ambao hawafanyi
mazoezi na sisi,” alisema Clichy.
“Kuna
juisi ameziondoa katika orodha, Pizza na vyakula vizito. Kuna watu huwa
wanadhani ‘Hilo ni jambo la kawaida na lazima iwe hivyo’ lakini ukweli ni
kwamba sio mara zote mambo yanakuwa hivi. Nimekuwa katika mpira kwa muda mrefu
na najua,” aliongeza beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Clichy
Mmoja
kati ya wachezaji ambao alirudi katika kambi ya City akiwa amezidisha uzito ni
kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Samir Nasri ambaye alipelekwa katika kikosi
cha vijana kufanya mazoezi.
Kwa
sasa Nasri ametolewa kwa mkopo kwenda katika Klabu ya Sevilla ya Ufaransa.
Guardiola
pia amewataka wachezaji wa timu hiyo wale chakula cha pamoja baada ya mechi zao
za nyumbani katika dimba la Etihad tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo
wachezaji walikuwa wanasubiriwa na wapenzi wao na kwenda kula nyumbani baada ya
mechi hizo.
Nasri
Kulikuwa
na utamaduni wa wachezaji wa City kulala katika hosteli za kisasa za timu hiyo
katika eneo la mazoezi lakini Guardiola amefuta utaratibu huo na badala yake
wachezaji kwa sasa wanalala na wake zao majumbani mwao siku moja kabla ya mechi
na kukutana siku ya mechi.
Post a Comment