MILAN, ITALIA
ROBERTO MANCINI
amevunja ukimya na kufunguka kile kilichotokea chini ya kapeti kati yake na
straika mtukutu Mario Balotelli wakati kocha huyo alipokuwa akiifundisha
Manchester City.
Kitendo hicho kilimpa
sifa mbaya kilitokea mazoezini baada ya kuzozana na Mario Balotelli mwaka 2013.
Mancini alinaswa na kamera akizozana na fowadi huyo Muitalino na
akiing’ang’ania kola yake.
Na sasa bosi huyo wa
zamani wa City amefafanua kwanini alikuwa
na hasira dhidi ya Balotelli.
Akizungumza na Gazeti la Ufaransa la
L’Equipe, Mancini alisema: “Katika mazoezi, niliwaambia wachezaji wasifanye
rafu za kijinga dhidi ya beki wa kushoto, Gael Clichy kwa sababu ndio kwanza
alikuwa ametoka kwenye majeraha.
Na baadaye, Mario alimfanyia rafu mbaya
sana dhidi yake. Nilikasirika.
Mancini akimvuta Balotelli.
“Nilimng’ang’ania
kwenye kola yake nilitaka kumsukuma lakini alikuwa na nguvu sikuweza. Kwa
kuziangalia picha unaweza kudhani labda tulipigana lakini hakukuwa na kitu kama
hicho.
“Aliingia (Balotelli)
kwenye ugomvi na baadhi ya wachezaji wenzake kwa sababu ya tabia yake, na
alikuwa akitaka kurudi Italia. Nilikasirishwa alitaka kuondoka kwa sababu
alikuwa na uwezo wa kufanya kitu kikubwa katika mashindano.”
Baada ya kushindwa
kutimiza majukumu yake Manchester City na kutimuliwa kwa mara ya pili AC Milan na
kushinda kufanya vizuri Liverpool sasa, Balotelli anafanya vizuri katika klabu
ya Ufaransa ya Nice.
Balotelli akimchezea rafu Clichy.
Hakuna anayehoji
kipaji cha Muitaliano huyo lakini siku zote amekuwa akiangushwa na tabia yake.
Baada ya kufanya
vizuri akiwa na timu ya taifa ya Italia katika mashindano ya Euro mwaka 2012 -straika
huyo hajachaguliwa tena katika timu hiyo tangu ilipomalizika michuano ya Kombe
la Dunia kule Brazili mwaka 2014.
Mancini ambaye
timu yake kuifundisha ni Inter Milan aliongeza: “Kama Mario leo hii haichezei
timu ya taifa ya Italia, ni juu yake. Ni jambo la kushangaza kwamba siyo fowadi
anayeanza katika timu yake ya taifa.
Wengine waliingilia kati kuamua.
“Ni straika bora wa
Italia katika miaka michache ya hivi karibuni. Nina matumaini Mario anafahamu
kwamba anapaswa kuwa na tabia tofauti na kufikiria soka tu. Haitakuwa vigumu
kwake.”
Mancini alikuwa na
matumaini makubwa kwa Balotelli alipokuwa City na alimwelezea kama mchezaji wa
ajabu baada ya kuifunga Manchester United mabao 6-1 na Balotelli akaonyesha
fulana yake aliyoiandika 'Why always me?’
Mancini aliongeza:
“Siku ile, ilikuwa kama Mario amezaliwa upya, alikuwa mkubwa na wengine
walikuwa watoto.
Balotelli akiwa Nice.
Ningependezwa kumuona siku zote akiwa kama alivyokuwa kwenye derby
ile, kwasababu vitu vilikuwa rahisi na vilikuja kama alivyokuwa akitaka yeye. Nilifurahi
alionyesha thamani yake.
Balotelli alipofanya kile kisichotarajiwa.
“Na hata alipoonyesha
fulana yake, kwa kweli nilijisemea mwenyewe kwamba ni mtu wa maajabu. Nani aliyefikiria
angefanya hivyo? Ni mtu wa maajabu kwa jinsi vitu vilivyokuwa vinakuja kichwani
mwake.”
Post a Comment