LONDON, ENGLAND
ARSENE WENGER kichwa kinamuuma kila anapofikiria jinsi wachezaji wake nyota wawili, Mesut Özil na Alexis Sanchez wanavyomwendesha mbio kama gari bovu.
kutokana na hilo, Arsenal itaingia gharama
zaidi ya Pauni 36 milioni baada ya kushinda kumalizana mapema na nyota hao, kwa kuwapa mkataba mpya katika usajili wa
majira ya joto.
Inadaiwa mastaa hao kila mmoja anataka kulipwa mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki ili kuweza
kuendelea kubaki uwanjani Emirates.
Wote Özil na Sanchez mikataba
yao inamalizika mwaka 2018 na klabu tayari imeshaandaa mikataba mipya na mirefu
kwa ajili ya wawili hao ambayo itaisha 2020.
Mbali na mastaa hao, Santi
Cazorla naye pia mkataba wake unakaribia kumalizika- ambao unatarajiwa kuisha
mwishoni mwa msimu- Bodi ya Arsenal imejaribu kufanya mazungumzo mara kadhaa, lakini
imekuwa ikirudi nyuma katika mazungumzo hayo na Özil na Sanchez.
Özil na Sanchez
Arsenal imepanga
kurudi katika meza ya mazungumzo baada
ya wachezaji hao kurudi kutoka katika michezo ya kimataifa, lakini mahitaji yao
ya Pauni 250,000 kwa wiki kutoka Pauni 70,000 ni zaidi ya kile
walichojadiliana mwaka jama.
Wenger
Siyo siri Özil na Sanchez ni wachezaji wa Arsenal wenye
thamani ndani na nje ya uwanja, na kwa viwango vyao msimu huu vimeisaidia
Arsenal kuwa katika ushindani wa taji la Ligi Kuu ikizingatiwa kwa sasa
inashika nafasi ya tatu, pointi mbili nyuma ya vinara Manchester City.
Mshahara mipya wanayohitaji
imekuja kama mshtuko kwa uongozi wa Arsenal, lakini kuna sababu tatu
zinazowafanya wahitaji mishahara hiyo.
Özil na Sanchez
Sababu mbili- zilikuliwa
zinatarajiwa na Arsenal, ni muda uliobaki kwenye mikataba yao kuelekea mwaka
mmoja mmoja na kuzua hofu ya kuondoka bure.
Sababu ya tatu ni mfumuko
wa bei katika mishahara ya Ligi Kuu England kutokana na dili jipya la matangazo
ya runinga mpango ambao umeleta athiri mwanzoni mwa msimu.
Post a Comment