BARCELONA, HISPANIA
XAVI HERNANDEZ hatimaye ameukubali mziki wa, Cristiano
Ronaldo baada ya kudai kwamba nyota huyo wa
Real Madrid atanyakua tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu.
Bila ya kutarajiwa kiungo
huyo wa kimataifa wa Hispania alianzisha vita vya maneno na Ronaldo Septemba mwaka huu baada ya kudai kwamba Ronaldo
hawezi kufananishwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi.
Ronaldo alijibu na
kujisifu kwamba yeye amechukua tuzo ya Ballon
d'Or mara tatu na kuzungumza kwa dhihaka uamuzi wa Xavi kwenda kumazia soka
lake Qatari katika timu ya Al-Sadd.
Hata hivyo, baada ya
majibu hayo ya Ronaldo, Xavi hakumjibu tena straika huyo wa kimataifa wa Ureno,
badala yake ameibuka upya na kudai kuwa Ronaldo atachakua mchezaji bora kwa
mara ya nne.
"Cristiano ana
nafasi kubwa ya kushinda Ballon d'Or mwaka huu, ameshinda Ligi ya Mabingwa na
Kombe la Ulaya ( akiwa na Real Madrid na Ureno)," alisema Xa vi .
"Lakini
ninadhani kutakuwa na ushindani, kwa sababu Messi atakuwapo pale, bila shaka."
Mgogoro kati ya wachezaji hao wawili
yalizuka baada ya Xavi kutakiwa kuwalinganisha Ronaldo na Messi katika
mahojiano."Ronaldo ni mchezaji wa muda huu," alisema, " lakini tatizo kuna mchezaji mwingine ambaye ni bora zaidi katika historia.
"Ronaldo ni mchezaji wa ajabu lakini ukili nganisha Messi, kwangu mimi na kwa yeyote anayependa soka, unaweza kusema hawafanani."
Alipoulizwa Ronaldo alijibu: "Sijali alichokisema Xavi kuhusu mimi, anacheza Qatar ambako sijui hata ni wapi.
"Ameshinda kila kitu, pamoja na Kombe la Dunia, ubingwa wa Ulaya, lakini hajashinda Ballon d'Or."
Agosti mwaka huu, Ronaldo alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ulaya mbele ya mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Gareth Bale na nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann.
Mwaka huuu Tuzo ya Ballon d'Or itapigiwa kura na waandishi wa habari baada ya Fifa kumaliza ushirikiano wa miaka sita mwezi Septemba na waandaji wa tuzo hiyo kutoka Ufaransa.
Uhusiano huo wa Ballon d'Or na Fifa ulimfanya Mchezaji Bora wa Dunia kuchaguliwa na waandishi wa habari, manahodha wa timu za taifa na makocha kwa miaka sita,.
Hata hivyom Fifa haijatangaza mipango yao ya kuchagua mchezaji bora wa dunia mwaka huu.
Post a Comment