MADRID, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO ni
tatizo kubwa ndani ya Real Madrid ndivyo anavyoamini Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England, Muitaliano, Fabio Capello.
Capello anasema Mreno
huyo hayupo kwenye kiwango chake na tabia yake ya upayukaji itaipoteza timu
hiyo.
Huo ni mtazamo wa bosi
huyo wa zamani wa Real, Capello ambaye anadhani Ronaldo hayuko sawa baada ya
kukosekana mwanzoni mwa msimu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Kocha huyo mkongwe wa
Italia alisema: “ Tatizo la Real Madrid kwa sasa ni Cristiano Ronaldo, kwa
sababu hayuko sawa kimwili na ndiye mchezaji wao bora.”
Straika huyo
ameiongoza klabu yake katika matokeo ya ajabu na na kuwa na malengo na alifanya
kazi ya kiwango cha juu katika misimu kadhaa lakini hajafanya jambo lolote la
maana hadi sasa katika msimu huuu.
Ronaldo akiwa msambweni
Kwa maelezo ya wazi
zaidi, inaonekana Ronaldo hajapona kimamilifu jeraha lake la goti baada ya
kuumia katika fainali ya Euro 2016.
Katika fainali hiyo
dhidi ya Ufaransa alilazimikan kutoka nje baada ya kukutana na changamoto na
kiungo Dimitri Payet aliyemumiza goti, ingawaje Ronaldo alifarijika baada ya
kuishuhudia Ureno ikitwaa taji.
Kocha Capello
Real Madrid
imeshindwa kuvuna pointi tatu katika michezo mine mfululizo, zote ikiambulia
sare, na mchezo wa karibuni ulikuwa dhidi ya Eibar.
Mbali na Eibar ambapo
Madrid ilipata sare ya bao 1-1, sare nyingine ni dhidi ya Dourtmund (2-2)
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Las Palmas 2-2 na dhidi ya Villareal 1-1.
Ronaldo akisikitika kukosa bao
Kocha Capello anaamini
mara Ronaldo atakapokuwa fiti, kikosi cha Zinedine Zidane kitarejea katika
ubora wake.
Katika msimu huu,
mpaka sasa Ronaldo amecheza dakika 318, amefunga bao moja na ametoa asisti moja
huku akitolewa uwanjani katika michezo minne.
Post a Comment