LONDON, ENGLAND
JOSE MOURINHO amesema itakuwa bure kuendelea
kuitwa ‘Special One’ kama atashindwa kutwaa mataji akiwa na Manchester United.Mreno huyo aliyejifunga mkataba Manchester United hadi 2020 mwezi Mei akichukua nafasi ya Louis van Gaal, alijipachika jina la Special One wakati akiwasali England kwa mara ya kwanza kuwa bosi wa Chelsea zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Akizungumza wakati akiwa anarejea Stamford Bridge Jumapili hii akiwa kocha wa United, Mourinho alisema mashabiki wa United hawatamuona wa maana kama atashindwa kuwapa mafanikio Old Trafford ndani ya miaka mitatu ijayo.
Mourinho alisema: "Muunganiko huanza kabla ya kushinda mataji lakini mafanikio ndio huleta maelewano kati ya mashabiki na kocha na kuufanya muunganiko huo kuwa wa kweli na wenye nguvu.
"Nina mkataba wa miaka mitatu hapa na kama nitaendelea kuwepo kwa miaka mitatu watu watajua nimeifanyia nini klabu na mimi ni mtaalamu na kocha ninayejiotoa saa 24 kwa ajili ya United.
"Lakini kama, mwishoni mwa miaka mitatu, kama sitakuwa na kipande kidogo cha medali kwa ajili yao, watasema 'mtu mkubwa, kocha mzuri, tunampenda, lakini hakuna kitu maalumu kutoka wake.'"
Jumapili itakuwa mara ya kwanza kwa Mourinho kwenda Stamford Bridge kama kocha wa klabu nyingine ya Ligi Kuu England.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53-alifukuzwa kwa mara ya pili akiwa kocha wa Chelsea mwishoni mwa Disemba kutokana na timu kufanya vibaya lakini kabla ya hapo, aliiongoza Chelsea kutwaa mataji manane yakiwemo matatu ya Ligi Kuu England, amekuwa akijivunia kile alichofanikiwa na klabu hiyo ya Magharibi mwa London.
Pia, Mourinho anafurahia uhusiano wake mzuri aliokuwa nao na mashabiki wa Chelsea, ingawaje kwa sasa anasisitiza yeye ni United kwa asilimia100.
Mashabiki wa Chelsea walipokuwa wakimsapoti Mourinho.
Alisema: "Chelsea imeshinda mataji manne ya Ligi Kuu katika historia yake. Matatu imechukia ikiwa na mimi na lingine moja imeshinda ikiwa na timu niliyoicha.
"Nimewapeleka Wembley, nimewapeleka Cardiff, nimewapeleka kwenye fainali za makombe. Kwa hiyo kuna muunganiko uliojengwa kutokana na uelewa- uliojengwa na mafanikio.
"Mwisho wangu ndani ya Chelsea, katika miezi miwili au mitatu wakati nikiwa na klabu kilikuwa kipindi cha matokeo mabaya, mashabiki walikuwa waelewa na kukumbuka uhusiano wetu.
"Hicho ni kitu ambacho sitakisahau na ni kitu ambacho kila siku nitakikumbuka kutoka kwao, kwangu, kila siku watakuwa wananichukulia tofauti.
“Nimeipenda kila klabu niliyoofanyia kazi. Nimekuwa na moyo huo wa kitalamu ambao unaniunganisha na klabu kwa asilimia 101.
"Wakati nilipokuwa nikikua Ureno, sikuwa shabiki wa Porto- lakini bado niliyatoa maisha yangu kwa ajili ya Porto. Pia nilijitoa kwa (Real) Madrid, niliyatoa kwa Inter Milan na Chelsea. Sasa nimeyatoa maisha yangu kwa United. Hiyo ni asili yangu. Kwa hiyo sasa ni United kwa asillimia 100."
Man United inatua London ikiwa katika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi14 baada ya michezo minane, pointi mbili nyuma ya Chelsea.
Kikosi hicho cha United kitacheza mchezo huo bila ya nahodha wake, Wayne Rooney ambaye aliumia mazoezini.
Post a Comment