0


LONDON, ENGLAND
ANTONIO CONTE ameangua kicheko baada ya kuzagaa kwa taarifa za uvumi kwamba yuko hatarini kutimuliwa klabuni Chelsea.
Hata hivyo, kocha huyo amedai kwamba anafurahia uhusiano mzuri kati yake na uongozi wa klabu hiyo.
Alhamisi kampuni moja ya wacheza kamari iliibuka na kusisitiza kwamba kuna uwezekano mkubwa kocha huyo Muitaliano huyo kupoteza kibarua chake Stamford Bridge, baada ya miezi mitatu tangu achaguliwe na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ili kufufua matumaini na ya klabu hiyo.

Conte akiwa amefadhaika.
Klabu ya Chelsea imefanya haraka kukanusha madai hao, na mmoja wa watu wa ndani ya klabu hiyo alisema : “Conte kupoteza kibarua chake ni ujinga."
Na kocha huyo Muitaliano alifanya mkutano na waandishi wa habari katika viwanja vya mazoezi vya timu hiyo, Cobham Ijumaa na kuzungumzia hilo.
"Najaribu kuangali nani ataweka fedha yake juu ya hilo," huku akicheka Conte alisema:
"Ni vigumu, kwa hilo. Ni gumu kuzungumzia kuhusu hali hiyo kwa sababu ninaangalia kuhusu kazi yangu, kuisaidia timu. Nina mawasiliano na uhusiano mzuri na klabu. Hakun kitu, hakuna kitu... nalipokea hilo kwa tabasamu."

Tajiri wa Cheslea, Abromovich 
Tetesi za kutimuliwa kwa Conte zilizagaa wakati wa mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa, baada ya tajiri, Abramovich kuzuru Cobham siku tatu mfululizo ndani ya wiki baada ya timu hiyo kufungwa na Liverpool na Arsenal.
Abromovich alikuwa alifika mara kwa mara katika mazoezi ya timu hiyo na kufanya mazungumzo na Conte.

Conte alipokuwa akiinoa Italia.
Lakini tajiri huyo wa Kirusi alikuwa na nia ya kuisapoti kuliko kumsimamia Conte, na Chelsea ilifanya vizuri na kuifunga Hull City 2-0 katika Uwanja wa KCOM mwanzoni mwa mwezi na kuweka rekodi nzuri katika msimu ikiwa katimu mabadiliko ya mfumo wa 3-4-3.
Mapumziko hayo ya mechi za kimataifa yalishuhudia kocha wa kwanza wa Ligi Kuu wa Swansea, Francesco Guidolin akifukuzwa na nafasi yake kurithiwa na Bob Bradley.
Na Conte alisema alikuwa tayari kuyakabili mashinikizo alipokubali kufanya kazi England.

Conte mazoezini Chelsea.
"Presha iko sawa na ile ya Italia," Conte aliongeza. "Ni kawaida. Ni kawaida kuishi kwa presha. Wachezaji wanaishi hivyo pia. Pindi unapokuwa katika klabu, unataka kushinda. Unataka kufanya kazi nzuri.
“Presha ni sehemu ya kazi yetu. Ni kawaida. Nafikiri ni sawa na katika nchi nyingine."

Post a Comment

 
Top