LONDON, ENGLAND
ROMAN ABROMOVICH (pichani chini) amepagawa
baada ya mambo kwenda mrama ndani ya Chelsea.
Kutokana na hali hiyo
bilionea huyo Mrusi anayelimiliki Chelsea amekutana na kocha wake, Antonio
Conte kwa siku tatu mfululizo na kula naye chakula cha mchana huku akijidiliana
naye jinsi ya kupata ufumbuzi wa kuifanya klabu hiyo kutoa ushindani katika kusaka taji la Ligi
Kuu- na jinsi ya kukijenga upya kikosi hicho.
Mwanzo mzuri wa
Chelsea ulikutana na ufa wa kutisha uliodhihirishwa na Liverpool na Arsenal katika
michezo miwili ya ligi, na ripoti inasema kibarua cha Conte kipo chini ya
uchunguzi wa bilionea huyo.
Taarifa zinaongeza
kwamba, Abromovich alikuwa kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo vya Cobham
kwa siku tatu mfululizo, ikifanya mazungumzo jinsi ya kuijenga upya Chelsea
iweze kutoa upinzani kwenye ubingwa.
Wachezaji wengi
wanaounda kikosi hicho walikuwa ni sehemu ya wale waliotwaa ubingwa wakiwa na
kocha wa zamani, Jose Mourinho msimu wa 2014/15, lakini kushindwa kwa timu hiyo
kutafutwa wachezaji mbadala – kumeifanya Chelsea kuwa katika nafasi ya nane
katika jedwali la Ligi Kuu. Klabu hiyo iko nyuma kwa pointi nane nyuma ya
vinara Manchester City.
Baada ya kuhudhuria mazoezini Jumatatu na Jumanne, Abramovich alitua tena
katika viwanja hivyo Jumatano ambapo alijadili hali ya sasa ya klabu hiyo.
Abromovich
Ripoti zinasema Abramovich
ameshindwa kuchukua hatua dhidi ya Conte kutokana na uhitaji wake wa wachezaji
wapya, na anaelewa matatizo yaliyotokea ya kushindwa kuwanasa baadhi ya
wachezaji aliowataka katika dirisha la usajili la majira ya joto zaidi ya
kumnasa N’Golo Kante kwa dau la Pauni 30 milioni kutoka Leicester City.
Conte.
Straika Michy
Batshuayi alitafutwa na Mkurugenzi wa Michezo, Michael Emenalo, wakati beki David
Luiz na Marcos Alonso waliwasili dakika za mwisho baada ya klabu hiyo kushindwa
kusajili beki wa Napoli, Kalidou Koulibaly na Alessio Romagnoli kutoka AC
Milan.
Post a Comment