0


MUNICH, UJERUMANI
BASTIAN SCHWEINSTEIGER (pichani juu) usiku uliopita aliachana na soka la kimataifa kwa kuichezea mchezo wa mwisho timu ya taifa ya Ujerumani. 
Sasa kazi iliyobaki kwa kiungo huyo wa zamani wa Bayern Munich ni moja tu, kumshawishi Kocha Jose Mourinho kupata baadhi mechi za kucheza Manchester United.
Mpaka sasa Mjerumani huyo ameshindwa kumashawishi wake wake huyo mpya na amekuwa akiiangalia United mpya ikianza vizuri kampeni ya Ligi Kuu England.

...akiwa na kocha wa Ujerumani
Matumaini kwa Schweinsteiger yapo mwezi huu ambapo itaaanza michuano ya Europe League na Kombe la EFL ambayo yanaweza kufungua mlango kwake kupata muda wa kucheza.
Hata hivyo kama Shweinsteiger atashindwa kumashawishi bosi wake kumrudisha kwenye kikosi  itambidi kuangalia sehemu nyingine na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 anafungua mawazo ya kwenda Ligi ya Marekani (MLS).

Akizungumza na vyombo vya habari vya Ujerumani baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Finland, Schweinsteiger alisema:
"New York ni jiji kubwa, lakini nina mkataba na United hadi 2018 na mnaijua hali ya hewa ilivyo Old Trafford."
“Ni ndoto yangu kurudi Manchester United. Nina matumaini natapata tena nafasi ya kuisaidia timu."

Mourinho
Hata hivyo, haitakua rahisi kwa Mourinho kushawishika hasa linapokuja suala la mchezaji anayedhani haendani na mipango yake na kocha huyo hakufurahishwa na kitendo cha Schweinsteiger kutotafuta klabu nyingine katika kipindi hiki cha  usajili wa majira ya joto.

Post a Comment

 
Top