MUNICH,
UJERUMANI
SHOKODRAN
MUSTAFI (pichani juu) amewatia jakamoyo mashabiki wote wa Arsenal wa duniani baada ya kuumia
akiitumikia Ujerumani.
Beki huyo wa kati alipangwa katika
listi ya wachezaji wa Ujerumani waliokuwa wakimuaga Bastian Shweinsteiger
katika mchezo wake wa mwisho wa kimataifa dhidi ya Finland, lakini aliondoka
uwanjani akiwa anachechemea kwa maumivu ya enka katika kipindi cha pili.Mustafi alikuwa anaweza kuendelea kucheza, lakini haikujulikana alikuwa ameumia kwa kiasi gani.
Mchezaji huyo wa zamani wa Everton amejiunga na Arsenal akitokea Valencia kwa dili la Pauni 35 milioni Jumanne, saa chache baada ya kukamilika kwa dili la straika wa Hispania, Lucas Perez.
Mustafi anatarajiwa kupangwa kucheza pembeni ya Laurent Koscielny sehemu ya ulinzi na kuwa moyo wa Arsenal msimu huu, lakini kupona kwake haraka kutaifanya Gunners kuwa imara.
Kocha Arsene Wenger anaamini hatakuwa na tatizo kubwa, ndio maana akalazimika kuwapanga Rob Holding na Calum Chambers katika mchezo wa nyumbani wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool na kuchezea kichapo cha mabao 4-3.
Beki Per Mertesacker atakuwa nje kwa muda mrefu na Gabriel Paulista pia anaendelea kuuguza majeraha.
Lakini Koscielny anarudi akiwa kamili na Wenger anatarajiwa hatapoteza muda wa kumpanga na Mfaransa huyo sambamba na Mustafi.
Post a Comment