0


LONDON, ENGLAND
BOSI mpya wa Ubelgiji Roberto Martinez amefanya usajili wa kushtukiza baada ya kumtaja mchezaji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry (pichani juu) katika benchi lake la ufundi la timu ya taifa ya Ubelgiji. 
Henry atachukua jukumu lake la kwanza la kuinoa timu ya wakubwa baada ya siku za nyuma kupata mafunzo akiwa na Arsenal. 

Martinez (katikati) ametaja kikosi chake.
 Mfaransa huyo awali alikuwa akikinoa kikosi cha chini ya miaka 18 cha Arsenal kabla ya kulazimishwa  kuondoka baada ya Arsene Wenger kumtaka aache kazi ya uchambuzi wa michezo katika Kituo cha Sky. 
Akiwa kocha wa Ubelgiji, Henry ataruhusiwa kuendelea na kibarua chake cha uchambuzi katika Kituo cha Sky  na atajiunga na timu ya taifa ya Ubelgiji katika msimu wa michuano ya kimataifa.

Henry (katikati) akiwa na Jamie Redknapp na  Jamie Carragher ataendelea na kibarua chake cha Sky.


Henry mwenye umri wa miaka 39- ataungana na bosi wa zamani wa Everton, Martinez na kocha  msaidizi anayeaminiwa, Mhispania, Graeme Jones. 
Tangazo hilo la Ijumaa la kushangaza lilitokea baada ya Martinez kutangaza kikosi chake tangu alipochukua jukumu la kuinoa timu hiyo baada ya michuano ya Euro 2016. 
Kwa maana hiyo, Henry atakuwafundisha mastaa wa Ubelgiji kina Eden Hazard, Marouane Fellaini na Kevin De Bruyne baada ya Martinez kutangaza kikosi kitakachocheza dhidi ya Hispania na Cyprus.

                              Fellaini  atafundishwa na Herny
Baada ya Kocha Martinez kumchagua Henry alisema: “Thierry amekuwa katika harakati za kubadilisha mfumo na ari kuwa katika utayari wa kutwaa mataji.”
“Nimetosheka kwamba (Shirikisho la Ubelgiji) lina uwezo wa kuwavutia wafanyakazi wake.
Imetangazwa kwamba kocha wa viungo, Richard Evans, ambaye kama Jones alimfuata Martinez  kutoka Swansea  na kujiunga na Everton baada ya kupitia Wigan, atakuwa katika majukumu kama hayo katika timu hiyo ya taifa.

kikosi kizima cha Ubelgiji
Henry aliandika katika mtandao wake wa Twitter: “ Nimepewa heshima kuchaguliwa kuwa kocha msaidizi. Shukrani kwa Roberto Martinez na Shirikisho la Soka la Ubelgiji. Nimesisikwa sana.  Sitaweza kusubiri.”
Mchezo wa kwanza wa Kocha Martinez akiitumikia Ubelgiji  utakuwa wa kirafiki dhidi ya Hispania Septemba Mosi ukifuatiwa wa ule wa ufunguzi wa  kuwania kufuzu Kombe la Dunia  dhidi ya Cyprus Septemba 6.

Post a Comment

 
Top