MANCHESTER,
ENGLAND
“JUAN
MATA ameonyesha kiwango chake halisi katika nafasi ya kiungo ndani ya kikosi
cha sasa cha Manchester United,” hayo si maneno ya mtu mwingine bali Kocha Jose Mourinho.Kocha Mourinho alisema Mata- ambaye anajipanga kusaini mkataba mpya na United-ni tofauti na yule aliyekuwa naye Chelsea.
Mourinho alimuuza Mata kwa United wakati alipokuwa kocha Stamford Bridge, Jumamosi iliyopita kiungo huyo alionyesha thamani yake kwa kufunga bao na ku-asisti wakati mabingwa watetezi Leicester walipofungwa mabao 4-1 uwanjani Old Trafford.
Kocha huyo Mreno alikuwa akizungumza, kuelekea mchezo wa Europa League Alhamisi dhidi ya Zorya Luhansk, alifafanua: "Chelsea tulikuwa tunachezaa kwa kujihami pindi tuliposhinda taji la msimu wa 2014-15.
Mata akishangilia moja ya mabao yake.
"Ni
jambo moja kuwa na wachezaji kwa ajili hiyo na wakati mwingine kuwa na
wachezaji wanaoweza kucheza kwa namna tofauti. Tunajaribu kucheza kwa namna
tofauti."Anaelewa kwa haraka na kwa ubora. Amekuwa na mazingira mazuri na halisi kwetu.
"Kwa maana hiyo Juan wa Chelsea katika mipango yangu ni kitu kimoja, na Juan katika mipango yangu Man United ni kitu kingine."
...akiwa na Mourinho.
Mourinho
alisema Mata, ambaye alijiunga na United kwa dau la Pauni 37.5 milioni na ameshaitumikia United katika michezo saba na kufunga mabao mawili msimu huu, "aliomba
kuondoka, Chelsea.
“Kwanza
kabisa sikumuuza,” Bosi huyo wa United alisema alipoulizwa kuhusu kuondoka kwa Mata
Chelsea Januari mwaka 2014.
“Kazi
yangu siyo kununua na kuuza. Kazi yangu ni kufundisha, kufanya kazi uwanjani na
kuishauri bodi kuhusu sera za uhamisho.
...Mata alimba mwenyewe kuondoka.
“Pili,
ni Mata mwenyewe ndiye aliyataka kuondoka na siku zote pindi mchezaji akiomba
kuondoka fikiria mara mbili. “'Na tatu fikra zangu za soka kwa kikosi
nilichokuwa nacho Chelsea ni kitu kimoja, na kikosi nilichonacho Man United na
wasifu na kile ninachojaribu kufanya katika klabu hii ni hali tofauti kabisa.
Post a Comment