0


LONDON, ENGLAND
MESUT OZIL (pichani juu) amezungumzia nia yake ya kutaka kuvaa jezi ya Arsenal No. 10 baada ya aliyekuwa akiimiliki kuondoka, wakati mazungumzo yake ya mkataba yakitarajiwa kuanza.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27- amechukua jezi namba No. 10 akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani baada ya Lukas Podolski kustaafu na amekiri angependelea kuwa na jezi yenye namba kama hiyo  uwanjani Emirates.
Jezi hiyo ndani Arsenal ilikuwa ikivaliwa na Jack Wilshere aliyejiunga na Bournermouth kwa mkopo wa msimu mmoja, Ozil anayevaa namba 11 alisema hiyo ni nafasi yake ya kuipata namba ambayo anaitamani.

...Ozil akiwa na Wilshere
"Itakuwa huru na nadhani bila ya shaka nitaipata," Ozil aliliambia Gazeti la Express la Ujerumani.
"Nilijaribu miaka michache iliyopita kuipata namba hiyo (Ujerumani), lakini Lukas Podolski aliizuia. Amecheza mechi nyingi zaidi yangu. Sasa imepatikana.
"Bila shaka, siku za nyuma niliwaonyesha ishara wote (Arsenal) kwamba nilikuwa nikiihitaji. Namba hiyo inanifaa na nafasi yangu kama mchezeshaji
"Kwangu, ina maana kubwa sana. Ni namba kipenzi changu. Wakongwe katika soka kama Zinedine Zidane, Diego Maradona na Pele walikuwa na namba hii migongoni mwao."
Ozil amebakisha miaka miwili katika mkataba wake Arsenal, lakini kumekuwa na tetesi kwamba Kocha Arsene Wenger anataka kumfunga mchezaji huyo kwa mkataba wa muda mrefu.

Ozil
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani pia anaamini kwamba mazungumzo na klabu yataanza muda si mrefu.
"Kwa sasa nataka kuangalia kuhusu timu ya taifa," Ozil alisema. "Sasa tutaangalia jinsi ya kuendelea na mazungumzo."
Katika mchezo ujao,Ozil anatarajiwa kurudi Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu uwanja wa nyumbani dhidi ya Southampton, baada ya mechi za kimataifa.

Post a Comment

 
Top