BUENOS
AIRES, ARGENTINA
LIONEL MESSI
amefichua siri iliyomfanya kupaka rangi nywele zake na kukana kumuiga beki wa
Manchester United, Phil Jones.
Muargentina huyo, 28, aliushtua
ulimwengu wa soka alipoonekanan amepata
rangi nywele zake mapema mwanzoni mwa msimu katika majira haya ya joto.Messi ambaye alitangaza kustaafu soka la kimataifa baada Argentina kufungwa kwa penalti dhidi ya Chile katika fainali ya Copa America sasa amerudi kwa kishindo.
Wiki hii aliisaidia Argentina kwa kupachika bao la ushindi dhidi ya Uruguay na kutangaza ujio wake kwa staili ya aina yake.
Straika huyo wa Barcelona amefafanua katika mahojiano kwamba matukio ya uwanjani katika majira haya ya joto yatakuwa bora kwake – na mabadiliko ya nywele ni sehemu ya kuonyesha kwamba ameanza upya.
Alifafanua: " Nimefanya mabadiliko na naanza kuanzia sifuri.
"Mengi yameendelea, mambo yametokea, na nikajisemea peke yangu: “Natakiwa kumaliza haya na kuanza tena.”
Ilikuwa vigumu kwa Messi kuvumilia kipigo cha fainali ya Copa America – na taarifa yake ya kustaafu ilionekana kuwa akili yake ilikubali kuwa ameshindwa kwa kuwa kipigo hicho cha Chile kilitokea mara mbili mfululizo.
Mwaka jana pia Argentina ilikosa taji hilo la Copa America mbele ya Chile kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
Mwaka 2004, Brazil timu hiyo ilifika fainali ya Kombe la Dunia na kufungwa na Ujerumani.
Messi aliendelea kufafanua: "Hivyo ndivyo nilivyokuwa nikijisikia wakati huo. Kila kitu kiliharibika. Nilijisikia hivyo kwamba (fainali) ilikiwa ni sehemu moja, kutokana na timu ilivyokuwa na jinsi tulivyocheza kwenye mashindano. Ilikatisha tamaa kwa kaisi kikubwa.”
Beki wa Manchester United, Phil Jones.
Messi ana kibarua cha kuhakikisha Barcelona
inatetea taji lake la La Liga msimu huu na kujaribu kushinda Ligi ya Mabingwa
linaloshikiliwa na Real Madrid.
Post a Comment