MADRID, HISPANIA
MINO RAIOLA (akiwa na Pogba pichani juu) ametengeneza zaidi ya Pauni
25 milioni za fasta katika dirisha hili la uhamisho la majira ya joto kwa
wachezaji watatu waliotua Manchester United, kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.
Wakala huyo wa soka,
ametengeneza fedha nyingi kuliko anazolipwa straika, Cristiano
Ronaldo katika mwaka mzima na Real Madrid.
Raiola mwenye umri wa
miaka 48-alimasaidia kiungo, Paul Pogba kuvunja rekodi ya usajili dunia kwa
Pauni 89 milioni ukiwa ni uhamisho kutoka Juventus kwenda Manchester United, na
pia alihusika katika kufanikisha dili la Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan kujiunga na klabu hiyo ya Premier
League chini ya Kocha Jose Mourinho ambaye alianza msimu wake wa kwanza Old
Trafford katika majira haya ya joto.
... akiwa na Ibrahimovic
Huko Pogba akiwa
mchezaji ghari wa soka duniani–akilipita
dau la Gareth Bale aliyetua Real Madrid kutoka Tottenham mwaka 2013 – Raiola alipata
ada ya uwakilishi kutokana na jukumu lake la kufanikisha dili hilo, na Gazeti la Hispania la AS limeripoti Mdachi huyo ‘superagent’ aliingiza
kiasi Pauni 16.8 milioni katika dili hilo.
Ronaldo
Hata hivyo, taarifa
za uhamisho wa Pogba hazikuwekwa wazi na Gazeti la The Independent linafahamu kwamba Raiola
anaweza kuwa aliingiza Pauni 24 milioni
kutokana uhamisho huo tu. Inakisiwa jumla aliingiza kiasi kinachokadiriwa kufikia Pauni 30 milioni katika majira ya
joto.
Mkhitaryan kazini
Ripoti inaweka wazi
kwamba Raiola alitengeneza Uero 8 milioni (Pauni 6.7 milioni) kutoka kwa Mkhitaryan
aliyetoka Borussia Dortmund, na Euro 3 milioni (Pauni 2.53 milioni) kutokana na
uhamisho wa Ibrahimovic, Msweden huyo
aliondoka bure kutoka Paris Saint-Germain.
Raiola
Jumla ya kiasi chote
ambacho United ilimlipa Raiola kinakadiriwa kufikia zaidi ya Pauni 32 milioni, wakati
mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi, Cristiano Ronaldo, anapokea Euro Uero 21milioni
(Pauni17.7milioni) kila msimu Real Madrid.
Post a Comment