NICE, UFARANSA
MARIO BALOTELLI (pichani juu) amempachika jina la ‘Mtu
mwenye Chuki za ajabu’ na ‘Mchezaji Mbaya’, mkongwe wa Liverpool, Jamie
Carragher baada beki huyo wa zamani kushangilia kuondoka kwa Balotelli Anfield wiki
iliyopita.
Straika huyo wa kimataifa
wa Italia hatimaye ameondoka Liverpool na kujiunga na Nice ya Ufaransa kwa ada
ya bure baada ya kutumia msimu uliopita akiwa kwa mkopo AC Milan, ambako
alifunga bao moja katika michezo 20.
Baada ya kutolewa bure,
Carragher alisema “bure ni malipo ya tabia mbaya.”
Carragher alishinda
Makombe ya FA Cups na makombe matatu ya ligi katika miaka yake 17- akiwa Merseyside
na akainua taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2005, sambamba na kucheza michezo 737.
Lakini Balotelli, ambaye
alikuwa mkali kwa wachezaji maarufu wa zamani wa Liverpool, alimjibu Carragher
kupitia mitandao ya kijamii.
Balotelli mwenye umri
wa miaka 26- aliandika: “Jamie Carragher, mchezaji mbaya, mwenye chuki za ajabu
@Carra23, nani anajali.”
Pia, alitupia picha ya
akiwa na taji na kuibebesha ujumbe “Mchukiaji Bora” na akaweka na picha zake
akishangilia mabao. Twiti hiyo ya Balotelli alipokea twiti nyingine 23,000
ndani ya saa 24.
Fowadi huyo wa zamani
wa Manchester City alijiunga na Liverpool akitokea Milan mwaka 2014 kwa dili la
Pauni 16 milioni- kuziba pengo la straika wa Uruguay Luis Suarez – lakini
alifunga bao moja katika msimu huo na kurudishwa kwa mkopo Italia.
Carragher
Carragher hakukaa
kimya kutokana na kitendo hicho cha Balotelli, kwani alimjibu kwa kumtakia heri
mchezaji huyo aende Nice na atwaye tuzo ya Ballon d’Or.
Post a Comment