0


TURIN, ITALIA
PAUL POGBA amewaacha hoi marafiki zake wa zamani wa klabuni Juventus wakiwa wamechanganyikiwa kwa kuvunja rekodi ya uhamisho baada ya kiungo huyo kutua Manchester United.

Pogba akiwa Man United
Uhamisho wa kiungo huyo Mfaransa kwenda Old Trafford ulikuwa ni habari kubwa katika dirisha la majira ya joto. Ulifikia mwisho baada ya United kukubali kutoa ofa ya Pauni 100 milioni kwa Juventus na kumwondoa kiungo huyo jijini Turin.
Baadhi ya wachezaji wa Juve wakiwamo Paulo Dybala na Gianluigi Buffon – wamesema Pogba aliwaambia kuwa atabaki klabuni hapo.
Kwa mujibu wa gazeti moja la Italia, klabu hiyo inahisi kama imesalitiwa na Pogba.
Dybala, anayeamiaminika kuwa ni rafiki wa karibu wa Pogba, alikuwa na huzuni wakati akizungumza na Gazeti la Malta wiki hii.

Dyabala
Muargentina Dyabala aliviambia vyombo vya habari na mashabiki kwamba: “Nina uhakika nitamuona Paul (Pogba) pindi tutakapostaafu.”
Gazeti hilo la Italia pia liliweka wazi kwamba Juventus haikuwa na mpango wa kuumuza kiungo katika majira haya ya joto.
Rais wa Juventus, Andrea Agnelli, na Mkurungeza Mkuu, Giuseppe Marotta walikuwa na nia ya kuendeleaa kuwa na  kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23- katika sehemu ya kikosi kwa ajili ya kampeni zinazokuja hasa Juventus akijipanga kuvunja rekodi ya kutwaa mataji mfululizo ya Serie A.

Buffon
Mabosi hao, Agnelli na Marotta walikuwa wanajipanga kumpa mkataba mpya Pogba ambao ungekuwa na ongezeko la ada ya usajili. 
Hata hivyo, dili la Pogba na United linaonekana ni nono kiasi kwa tofauti kubwa kuliko ofa ambayo Juventus ingetoa kumbakisha Pogba.

Pogba akimwaga wino, Man United
Juventus ilikuwa imepanga kumuuza kiungo huyo mwishoni wa msimu wa 2016-17, ikiamini kwamba ingepata ada kubwa zaidi kuliko kiasi ilichopata na kuvunja rekodi ya uhamisho kutoka United.

Post a Comment

 
Top