LONDON, ENGLAND
CHELSEA inapaswa
kujipanga ili kuwa na beki ngumu kama inataka kushindania ubingwa msimu huu,
kwa mujibu wa kiungo mshambuliaji, Eden Hazard (pichani chini).
Pamoja na kwamba
kocha mpya, Antonio Conte anaheshimika kwa kujenga ngome imara katika katika
timu mbalimbali, Chelsea imeruhusu mabao tisa katika Ligi Kuu England msimu huu,
yakiwemo matatu dhidi ya Arsenal Jumamosi iliyopita.
Bao la kwanza
uwanjani Emirates lilifungwa baada ya makosa ya beki wa kati, Gary Cahill na
wakati huo kiungo wake asiyechoka N'Golo Kante alikuwa akikimbiza nyuma na
mwamuzi Michael Oliver.
Kwa uhakika huo klabu
hiyo ya Magharibi mwa London haijafungwa bao katika mchezo mmoja tu katika
michezo sita ya ligi mpaka sasa.
“Kila wiki tumekuwa
tukitoka nyuma na kushinda. Tulifanya hivyo dhidi ya Leicester (katika Kombe la
Ligi) lakini dhidi ya Arsenal ambao walicheza nyumbani kwao, haikuwa rahisi,” alisema
Hazard.
...Hazard akipambana.
“Hakuna msamaha (kwa kipigo cha Arsenal). Haikuwa
kitendo kizuri. Tumepoteza mengi.”
Chelsea ambayo
haijapata ushindi katika michezo mitatu ya ligi, iko nafasi ya nane katika
msimamo wa ligi, pointi nane nyuma ya vinara Manchester City. Timu hiyo ikiwa
chini ya Muitaliano Conte, itacheza na mabingwa watetezi, Leicester City na
Manchester United katika mechi mbili kati ya tatu zinazofuata.
Beki Cahill baada ya kufungisha
“Tunahitaji kuwa bora.
Katika michezo mitatu ya mwisho ya ligi tulipaswa pointi tisa zilikuwepo na
tumepata moja. Inakatisha tamaa,” alisema kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji.
“Tunapaswa kwenda
kuyafanyia kazi makosa tuliyoyafanya kufuatia michezo mikubwa tunayokabaliana
nayo mbele ya safari.”
Kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil akiwanyanya Chelsea.
Katika mchezo ujao wa
ligi hiyo, Chelsea itasafiri kuifuata Hull City Jumamosi ijayo.
Post a Comment