LIVERPOOL,
ENGLAND
JURGEN
KLOPP (pichani chini) amefunguka kwamba hamu yake kubwa kama kocha wa Liverpool ni kuiona timu
hiyo ikipiga mpira mwingi na watu wakumbuke kwa miaka kadhaa.Liverpool imekuwa ikicheza soka la kuvutia machoni tangu kuwasili kwa Kocha Klopp, Oktoba 2015 na bosi huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amekuwa akiiongezea makali katika mfumo kupiga pasi.
Wekundu hao wameshaanza kufurahia ushindi wa kukumbukwa kwa baadhi ya timu bora katika Ligi Kuu England na Ulaya katika utawala wa Klopp, na anaamini kucheza soka la kukumbwa maana yake mafanikio yatafuata.
Klopp alikuwa akichati katika Mtandao wa Facebook na Sky Sports Jumatatau usiku, kocha huyo aliulizwa nini malengo yake makubwa akiwa kocha wa Liverpool, alisema: "Ni kucheza soka ambalo tutakuja kulikumbuka pindi tukiangalia nyuma.
"Hiyo ndio nia yangu na nafikiria hilo ndilo unalopaswa kulifanya katika maisha, kutumia muda wako pamoja kutengeneza kitu ambacho unaweza kukifurahia pindi unapoangalia nyuma, unafikiria kuwa labda ulikuwa na muda mchache ambao hukuwahi kuwa nao.
...Klopp katika mahojiano.
"Haiwezi
kutokea tukamaliza katika nafasi ya 15 tunapokuwa na wakati kama huo kutokana
na ubora tuliokuwa nao, hiyo haiwezekani."Kocha huyo Mjerumani aliongeza: "Lakini najua nini kila mmoja anataka kusikia kwa sababu kuna kimbilio kubwa katika soka na wengine wanataka kusikia tunataka kushinda taji la ligi.
Klopp akiwa na nahodha wa Liverpool.
"Bila
shaka tunataka kushinda hilo, sijui ni nini kitatokea, lakini ninaloweza kusema
tutafanya kwa uwezo wetu kama hatutakuwa mbali na timu kwenye vita ya kuwania ubingwa."
Post a Comment