0


BUENOS AIRES, ARGENTINA
CARLOS TEVEZ (katika picha tofauti chini) straika wa Boca Juniors ya Argentina amekiri kwamba anafikiria kustaafu kusakata soka mwishoni mwa msimu huu.
Tevez, 32, amekuwa alifikiria kustaafu baada ya Boca Juniors kutolewa katika nusu fainali ya Copa Libertadores na Independiente del Valle katika majira ya joto yaliyopita, lakini ameendelea kuitumikia klabu hiyo.
Straika huyo aliyewahi kutesa katika Ligi Kuu England akiwa na West Ham, Manchester United na Manchester City, ameibuka sasa na kudai Ligi ya Argentina ni maafa, hivyo anataka kustaafu.

"Hii inachosha," alisema Jumanne "Nitafanya mazungumzo na familia yangu na watu ambao nitahitaji kuzungumza nao. Ndio, nafikiria kustaafu, lakini nilipendelea kucheza katika maisha yangu yote katika klabu hii. Kufika Bombonera kila Jumapili kunanifanya niwe na furaha."
Wakati Boca ikiwa inajiandaa kupambana na Lanus, Jumatano katika raundi ya pili ya Copa Argentina, Tevez amelalamikia kufungiwa kwake mechi tatu-haikuwa haki na amevilaumu vyombo vya habari.

"Nafikiri adhabu hii nimepewa na waandishi na wala siyo kamati," alisema. "Waandishi wameshawishi nifungiwe mechi tatu, ni kweli itakuwa nimepigwa kofi. Kwa hiyo labda ni nzuri labda mbaya. Lakini tuliona wiki iliyofuata mwamuzi hakuwa makini na hilo lilinisumbua."
Pia, Tevez aliilamu ligi na wamiliki kwa kwa kuwa haifuati ratiba.

"Shirikisho lina hali mbaya. Ulaya mtu unajua tarehe mtakazocheza katika mechi za kwanza za miezi sita. Hapa huwezi kupanga chochote," alisema.
Straika huyo alisema hakufanya vizuri akiwa na Boca kiasi cha kuweza kuitwa kwenye timu ya taifa ya Argentina.
"Kile mchezaji anachokifanya klabuni ndicho kinachomfanya aweze kuitwa katika timu ya taifa," alisema Tevez. "Sijacheza vizuri tangu dakika ya kwanza dhidi ya Belgrano."

Mchezaji huyo wa zamani wa Juventus alisema anadhani mchezaji wa Inter, Mauro Icardi lilikuwa chaguo sahihi kwa sababu amefanya vizuri, amefunga mabao akiwa na Inter.
"Mwisho wa siku uamuzi ni wa kocha. Kocha Bauza hakuwa katika presha kuchagua mmoja baada ya mwingine. Anacho paswa kumchagua mmoja ambaye ni bora. 

"Sidhani kama ninastahili kuwa pale kwa sababu sijacheza vizuri na sijui kama ninapaswa kuondoka kwenye timu au la (kutokana na kufungiwa mechi tatu)."
Akiwa England, Tevez alizitumikia timu hizo tatu na kufunga jumla ya mabao 84  katika michezo 202.

Post a Comment

 
Top