MANCHESTER,
ENGLAND
MANCHESTER
UNITED imeivuruga heshima ya Real Madrid katika ufalme wa soko la usajili
duniani.
Maofisa kwa
klabu hiyo wanaamini wamefanya kitu kikubwa kwa kuwashinda Mabingwa wa Ulaya
kwa kumsaini Paul Pogba na kuweka rekodi ya dunia ya dili la Pauni110 milioni.
Real Madrid
iliweka rekodi tano za dunia, ikiwemo kumsaini nyota wa Ligi Kuu, Cristiano
Ronaldo kutoka United na Gareth Bale kutoka Spurs – ilipambana kumpata Pogba kutoka
Juventus na ofa yao ilikuwa sawa na ile ya United.
Hadi Jumanne
usiku miamba hiyo ya Old Trafford ilikuwa ikiendelea kushangilia kumnasa Pogba na
vyanzo vimekanusha kwamba Real ilifanya majaribio ya kumnasa Pogba chini ya
kiwango cha maslahi yao.
United inajivunia
mafanikio haya dhidi ya miamba hiyo ya Hispania na inasisitiza nguvu yao kubwa
na ile ya bosi wao mpya, Mourinho ndio iliyozaa mafanikio.
Nyota huyo
wa kimataifa wa Ufaransa, Pogba usajili wake umebadili mwenendo wa nyota kama
Luis Suarez, Ronaldo na Bale kuachanana Ligi Kuu kwa ajili ya La Liga, na United
ina furaha kuipiga bao Madrid kwa sababu
bosi wake Zinedine Zidane ni Mfaransa mwenzake na Pogba.
United
inafikiria, kuwasili kwa Pogba kumewapa
ushindi mara mbili dhidi ya Real baada
ya miamba hiyo ya Bernabeu kushindwa kumrubuni kumrudisha nyumbani (Hipsania) kipa,
David De Gea mapema kwenye msimu huu wa majira ya joto.
Mkongwe wa
United, Gary Neville anakiri kwamba kitendo cha Pogba kusaini ni ishara ya
kuhama kwa ushawishi wa nguvu kati ya
England na Hispania.
Neville
alisema: “Nadhani ni ada kubwa, lakini Ligi Kuu
imeshapoteza wachezaji wa kushoto, kulia
na wakatikati kwa Hispania – wote wachezaji wa daraja A.
“Hatukuweza
kuwashawishi wachezaji kuja hapa wakati sisi ndio bora. Sasa tumesajili
mchezaji ambaye anaonekana kuwa ndiye usajili mkubwa wa majira ya joto.”
Mchezaji wa
zamani wa Barcelona, straika Gary Lineker anadhani usajili wa Pogba ni mabadiliko
ya soko la usajili.
“Kusajiliwa
kwa Pogba na Man United kunamaanisha sasa ni wakati muhimu wa Ligi Kuu,” alisema.
“Kwa mara ya kwanza nyota mkubwa wa kigeni akiwa katika ubora wake ametua England.
"Miamba
mingine itakuja hapa na siyo tena kwa Barca na Real Madrid.”
Post a Comment