0
LONDON, ENGLAND
ARSENAL WENGER amekiri kuendelea kwake kuwa bosi wa Arsenal kwa mwaka unaofuata kutategemea matokeo ya msimu huu unaotarajiwa kuanza Jumamosi.
Lakini Mfaransa huyo ambaye mkataba wake unaisha mwakani katika majira ya joto, ameonesha kutakuwa na nia ya kustaafu hata kama akionodoka Arsenal.
Wenger amekuwa na umaarufu mkubwa Kaskazini mwa London, lakini huku klabu ikikosa mataji zaidi ya mwongo mmoja uliopita na kumfanya kuwa katika msuguano na mashabiki.

Na alipoulizwa kama ataongeza muda wa kuitumikia Arsenal, Wenger alijibu: “Nini nitafanya kitategemea kwa kiasi kikubwa na jinsi msimu utakavyokwenda.”
Wenger alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kumrithi  kocha wa England, Roy Hodgson baada ya timu hiyo ya taifa kuvurunda Euro 2016, lakini bosi huyo wa Gunners hakuwa amejiandaa kuvunja mkataba wake.
Lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 66, akizungumza katika uzinduzi wa Ligi Kuu, alidokeza atafungua mlango wa kufanya kazi sehemu nyingine siku zxa baadaye na hana lengo la kustaafu.

...mashabiki wanaompinga Wenger.
“Kitu nitakachofanya ni kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu kadiri nitavyokuwa na uwezo wa mwili wa kufanya hivyo, bila ya kujali nitakuwa katika nafasi gani,” aliongeza Wenger.

“Kila siku nitakuwa nikifanya kazi. Unapaswa kufanya hivyo hata kama katika maisha yako yote, lakini ukiwa unajua unaweza kuacha wakati wowote.”

Post a Comment

 
Top