0
LEICESTER, ENGLAND
CLAUDIO RANIERI amemwaga wino kutumikia Leicester City hadi mwaka 2020.
Ranieri ambaye aliingia dili la miaka mitatu pindi alipokuwa akirithi mikoba ya Nigel Pearson kuwa kocha wa majira ya joto mwaka jana, ameiongoza Leicester kutwaa taji la Ligi Kuu katika msimu wake wa kwanza kazini.
Bosi huyo wa zamani wa Chelsea, Juventus na Monaco aliuaambia mtandao wa klabu hiyo  Jumatano: "Wakati nilipokuwa nikizungumza na na wamiliki kuhusu mtazamo wao kwa Leicester City, nilifahamu ni kitu ambacho ninachotaka kuwa sehemu yake kwa muda mrefu.
"Nguvu inayodumu katika klabu hii – kutoka kwa wamiliki na wafanyakazi, wachezaji na mashabiki- ni kitu fulani maalumu sana. Nina furaha na ninajivunia  kwamba nitakuwa sehemu ya kitu hicho kwa miaka kadhaa inayokuja.
"Msimu uliopita, nguvu na kujituma ilitusaidia kutupa mafanikio. Kama tutaendelea kujituma, kudumisha shauku yetu na kuendelea kupambana kwa mioyo yetu, nina uhakika tutaendelea kupata mafanikio pamoja."

Ranieri alichaguliwa kuinoa Leicester baada ya kufukuzwa Ugiriki, na busara zake zimempa Mtaliano huyo mafanikio uwanjani King Power Stadium, lakini matarajio yake yalikuwa makubwa alipokuwa akirudi Ligi Kuu England.
Makamu Mwenyekiti wa Leicester, Aiyawatt Srivaddhanaprabha amesema: " Miezi 12 iliyopita, tulimleta Leicester City mtu mwenye maarifa na uzoefu, tuliona anaweza kutupeleka katika awamu ya pili ya mipango yetu ya muda mrefu.
"Kitu gani ataendelea kutupatia, katika kipindi ambacho tayari tuna mafanikio, kimekuwa ni zaidi ya kitu chochote tunachoweza kukitarajia.

"Sifa za Claudio, akiwa kama binaadamu na kama kocha, zimekuwa wazi tangu alipowasili – Sifa ambazo zimeisaidia Leicester City kupata maendeleo katika kila ngazi. Tuna msingi mathubuti sana katika kuifanya klabu yetu kuwa na maendeleo, na nina furaha kwamba Claudio ataendelea kuwa sehemu ya safari hiyo."
Mkurugenzi Mtendaji wa Leicester, Susan Whelan amesema: "Nadhani ni muhimu sana katika suala la utulivu.
"Alikuwa na faida kubwa katika kila kipengele cha klabu. Tabia yake, utu wake umekuwa muhimu sana.”

Post a Comment

 
Top