0


MADRID, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO hatimaye amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Real Madrid- hayo yamefichuliwa na rafiki wa karibu wa straika huyo, Conor McGregor.
Maisha ya baadaye ya Mreno huyo ndani ya Bernabeu yalikuwa chini ya uangalizi baada ya mkataba wake kubakisha miaka miwili kumalizika.

Lakini Ronaldo aliwaomba mabosi wa Real Madrid kuongeza mkataba wake baada ya kuingoza klabu hiyo katika kushinda taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita- na inaonekana maombi ya supastaa huyo yamekubaliwa.
Gazeti la AS lilidai mwezi uliopita kwamba Ronaldo alikuwa akijipanga kusaini mkataba mpaka mwaka 2020 au 202, katika kumalizia soka lake la Ulaya na Real.
Lakini mchezaji wa ngumi za kwenye vizimba (UFC), McGregor, ambaye ni rafiki wa karibu wa Ronaldo amefichua moja ya siri kubwa katika soka duniani.

McGregor 
 Alipoulizwa kama ataweza kuwa na nafasi ya kumpita Ronaldo katika wanamichezo watakaotajwa Jarida la Forbes, McGregor alisema: “Hiyo itakuwa kazi ngumu.”
“Hivi karibuni amesaini mkataba mpya na Real Madrid lakini tutaangalia, labda mwakani nitaweza kumshinda,” alijibu MC Gregor.

Ronaldo alimtembelea McGregor katika mazoezi yake mapema kipindi cha majira ya joto.
Gazeti la AS limedai habari hizo zitatangazwa kabla ya mapumziko ya kimataifa Agosti 29.
Ronaldo atakuwa na uwezekano mkubwa wa kuitwa katika mchezo wa kirafiki kati ya Ureno  dhidi ya Gibraltar, na Real bila ya shaka itapanga sherehe mbele ya mashabiki wake kusherehekea makubaliano hayo.

Post a Comment

 
Top