BOURNERMOUTH, ENGLAND
ZLATAN IBRAHIMOVIC amepachika bao
katika mchezo wake wa kwanza wa ugenini wa Ligi Kuuu wakati kikosi hicho cha
Jose Mourinho kilipoanza kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth.Kiungo, Juan Mata na Wayne Rooney waliingia katika hesabu ya ufungaji.
Ibra akishangilia.
Hata hivyo katika kipindi cha kwanza
kilikuwa cha kukatisha tamaa baada ya Manchester United kupoteza fursa kadhaa
za kupata bao la mapema.Bao la kwanza la United lingepatika kabla ya nusu ya kwanza baada ya Mata kumpasia mpira Rooney, lakini jitihada za straika huyo zilikosa nguvu na kuishia katika mikono ya kipa wa Bournemouth, Artur Boruc.
Kocha Mourinho, akishangilia na wachezaji wake.
Kiungo wa Bournermouth, Harry Arter alipiga
mkwaju wa mita 35 katika jitihada za
kutaka kufunga lakini haukuzaa matunda.United ilichukua uongozi dakika tano kabla ya mapumziko, lakini zilihitajika jitihada za makosa ya beki wa Bournemouth defender ili kuweza kupata bao hilo.
Mata akifanya vitu vyake.
Beki, Simon Francis aliurudisha pasi
fupi kwa kipa Boruc na kumwezesha Mata kuuwahi-
Boruc aliucheza kumzuia Mata kufunga lakini ulimgonga tena Francis na kumerudia
Mata aliyeupachika wavuni.
Mata huyooo...
Straika Rooney angeza kupachika bao
la pili dakika sita baada ya mapumziko baada ya kumzidi misuli beki Steve Cook na
kuelekea golini, lakini Boruc alizuia juhudi hizo.Dakika chache baadaye Rooney aliodai penalti baada ya kupambana na Andrew Surman- hata hivyo katika marudio ya runinga ilionekana ni tukio la kawaida.
Rooney alibadili matokeo katika dakika 59 baada ya kuipa United bao la pili. Antonio Valencia alipasua njia upande wa kulia na kupiga krosi kwa Anthony Martial, aliyejaribu kufunga na mpira kumkuta Rooney akiwa yadi sita kutoka langoni mwa Bournemouth.
Rooney akifunga
Mpira wa nguvu wa adhabu uliopigwa
na Ibrahimovic ulizuiiwa na kipa Boruc.Lakini dakika chache baadaye, Msweden huyo alifunga likiwa bao la tatu. Kabla ya mchezo huo Ibrahimovi alifunga bao katika mchezo wa Ngoa ya Jamii dhidi ya Leicester.
Aliupata mpira akiwa yadi 25 kutoka umbali wa goli na kuupiga mpira katika engo tofauti kwa shuti ambalo halikuwa na nguvu sana.
Rooney akishangilia.
Bao la Bournemouth lilifungwa na
katika dakika ya 69 na Adam Smith aliyetokea
benchi.
Francis na Smith wakishangilia bao lao.
Post a Comment